IQNA

Baraza la Usalama UN laidhinisha muswada wa kuunga mkono Afghansitan

12:24 - December 23, 2021
Habari ID: 3474712
TEHRAN (IQNA)- Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamepitisha kwa kauli moja azimio la kurahisisha shughuli za upelekaji misaada nchini Afghanistan.

Baraza la Usalama UN laidhinisha muswada wa kuunga mkono AfghansitanAzimio hilo limejuzisha ulipaji fedha, utoaji mali katika sura ya fedha au vyanzo vya kiuchumi, bidhaa na huduma zinazohitajika ili kuhakikisha misaada ya kibinadamu inatolewa kwa wakati au kusaidia na kuunga mkono shughuli za aina hiyo nchini Afghanistan.

Halikadhalika, azimio hilo lililopitishwa na Baraza la Usalama la UN limemtaka mratibu wa misaada ya dharura wa ofisi ya uratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA awasilishe ripoti mara moja kila baada ya miezi sita kwa baraza hilo kuhusu upelekaji misaada ya kibinadamu nchini Afghanistan ikiwemo kuwapatia fedha watu au asasi zilizoainishwa.

Ripoti ya mwisho kuhusu hali ya chakula nchini Afghanistan, ambayo ilitolewa mwezi Oktoba ilitahadharisha kwamba kuanzia Novemba 2021 hadi Machi 2022 watu milioni 22.8 watakabiliwa na hali mbaya au kiwango cha upeo wa dharura wa kutokuwa na uhakika wa kupata chakula nchinii Afghanistan. Idadi hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 35 kulinganisha na kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Mnamo mwezi Septemba mwaka huu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa mwito wa kuchangishwa msaada wa dola milioni 606 kwa ajili ya kuwapatia misaada ya kibinadamu Waafghanistan milioni 11 katika sekta kadhaa, ikiwemo ya usalama wa chakula, kilimo, elimu katika mazingira ya dharura, afya na siha na lishe na upatiaji hifadhi.

4022940

captcha