Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Kenya, Sheikh Abdillah Nassri alifariki jana asubuhi mjini Mombasa na alizikwa siku hiyo hiyo Alasiri katika Maziyara ya Wakilindini Mombasa baada ya kusaliwa katika Msikiti wa Hassanaina maarufu kama Bahman.
Sheikh Abdillahi Nassir alikuwa mfuasi wa madhehebu ya Ahul Bayt wa Mtume Muhammad SAW na alipata umaarufu kama mwanazuoni, mwalimu, mhadhiri na mwandishi maarufu wa Kiislamu mbali na kuwa miongoni mwa wajumbe wa Kenya katika mazungumzo ya kupigania uhuru ya Lancaster huko London mwaka 1960
Marehemu alikuwa mwanachuoni mcha Mungu,mvumilivu, mnyenyekevu na mpambanaji katika njia ya Mwenyezi Mungu na hakuacha kushauri, kutoa muongozo na maelekezo hadi mwisho wa uhai wake.