IQNA

Hauli ya Sheikh Abdillahi Nassir, mwanachuoni mtajika wa Kiislamu Afrika Mashariki

21:54 - March 08, 2022
Habari ID: 3475024
TEHRAN (IQNA)- Hauli ya marhum Sheikh Abdillahi Nassir, mwanachuoni mtajika wa Kiislamu Afrika Mashariki imefanyika mjini Nairobi, Kenya.

Januari 11 2022 ilikuwa siku ya huzuni kwa Waislamu wa Afrika Mashariki na Ulimwengu wa Kiswahili kwa kuondokewa na Sheikh Abdillahi Nassir, aliyekuwa mwanazuoni nguli wa Taaluma za Kiislamu na lugha yetu aushi ya Kiswahili.

Kwa mnasaba huo, hauli imefanyika mjini Nairobi Jumapili na kuhudhurwa na Waziri wa Utalii wa Kenya Najib Balala na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya Jaafar Barmaki. Aidha wasomi wa Kiislamu kutoka maeneo mbali mbali ya Kenya wamshiriki katika hauli hiyo.

Mwanazuoni huyu mtajika aliandika vitabu mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza, vilivyosaidia pakubwa kujenga na kukuza imani za Waislamu. Baadhi ya vitabu hivyo vimefasiriwa kwa kadhaa za kigeni.

Katika miaka ya karibuni amekuwa akijishughulisha na uandishi wa tafsiri ya Qur’ani Tukufu kwa lugha ya Kiswahili na kueneza mafundisho ya Ahlul Bayyt (as). Miongoni mwa vitabu vya marehemu Sheikh Abdillahi Nassir ni Shia na Qur'ani, Maulidi si Bidaa, Si Haramu, Ukweli wa Hadithi ya Kisaa, Mut'a Ndoa Halali, Ukweli wa Hadithi ya Karatasi, Ahlul Bayt Ni Nani? na Yazid Hakuwa Amirul Muuminin.

Hauli na vikao mbali mbali vya Khitma ya marhum Sheikh Abdillahi Nassir vinaendelea kufanyika Kenya na Tanzania na maeneo mengine duniani.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

4041286

captcha