IQNA

15:59 - January 16, 2022
Habari ID: 3474815
TEHRAN (IQNA)- Maonyesho kuhusu uchapishaji Qur'ani Tukufu yamezinduliwa Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia.

Maoneysho hayo yameandaliwa na Wizara ya Masuala ya Kiislamu, Dawah na Muongozo kwa ushirikiano na Kituo cha Uchapishaji Qur'ani cha Mfalme Fahd,

Kwa mujibu wa taarifa maonyesho hayo yamefunguliwa rasmi Alhamisi Januari 13 na yataendelea kwa muda wa siku 10.

Vibanda kadhaa vimewekwa nje ya ujumbi wa maonyesho ili kuwahimiza watu zaidi waweze kuingia katika maonyesho hayo ya Qur'ani.

Kituo cha Uchapishaji Qur'ani cha Mfalme Fahd  huchapisha misahafu takribani milioni 10 kwa mwaka na hadi sasa kimechapisha tarjuma ya Qur'ani Tukufu kwa lugha 39 duniani.

 

4028625

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: