IQNA

Maonyesho ya Qur'ani

Maonyesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur’ani yafunguliwa Tehran

15:00 - March 21, 2024
Habari ID: 3478552
IQNA - Toleo la 31 la Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yalizinduliwa rasmi katika hafla ya Jumatano jioni, Machi 20.

Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu Iran Mohammad Mehdi Esmaeili ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyoanza qiraa ya Qur’ani ya qarii mashuhuri wa Iran, Ustadh Hadi Movahed Amin.

Katika hotuba yake, Esmaeili alipongeza uzinduzi wa maonyesho hayo katika siku ya kwanza ya msimu wa machipuo na katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Aidha amekaribisha ushiriki wa wanaharakati wa Qur'ani kutoka nchi 25 katika hafla hiyo ya kimataifa.

Waziri wa Utamaduni pia alibainisha kuwa katika Ramadhani, maonyesho mengine 30 ya Qur'ani yamewekwa au yatawekwa katika majimbo 30 kote Iran.

Ameongeza kuwa wizara hiyo imefanya juhudi kubwa za kuimarisha mazingira Qur'ani katika jamii katika mwezi huu uliobarikiwa.

Wizara ina mpango wa kukuza usomaji wa Qur'ani, usomaji na kuhifadhi na kueneza dhana za Qur'ani katika maisha ya watu wote nchini, aliendelea kusema.

Kwingineko katika matamshi yake, Esmaeili ameashiria muqawama yaani Mapambano ya Kiislamu ya wananchi wa Ukanda wa Gaza dhidi ya utawala ghasibu wa Israel na akinukuu aya za Qur'ani Tukufu, akasisitiza ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kuwasaidia wale wanaoendelea kuwa na msimamo thabiti katika kukabiliana na dhulma na dhulma.

Shobeyr Firouzian, Naibi Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu anayesimamia Qur'ani na Etrat ambaye pia ni mkuu wa maonyesho hayo pia alihutubia sherehe hiyo, akifafanua vipengele tofauti vya maonyesho ya mwaka huu.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kukuza dhana za Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani nchini Iran.

Aidha huwa jukwaa la kuomnyesha afanikio ya hivi punde zaidi ya Qur'ani nchini Iran na pia bidhaa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

4206537

Habari zinazohusiana
captcha