IQNA

Ibada ya Hija

Misahafu nusu milioni yasambazwa Makka wakati wa Hija

15:48 - July 07, 2022
Habari ID: 3475471
Zaidi ya nakala nusu milioni za Qur'ani Tukufu zimesambazwa katika Msikiti Mtakatifu wa Makka, Al Masjid al Haram na maeneo matakatifu karibu na mji huo, Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia imetangaza.

Ilibainisha kuwa nakala hizo zimechapishwa na Jumba la Uchapishaji Qur'ani Tukufu la Mfalme Fahd lenye makao yake Madina.

Aidha nakala hizo za Qur'ani zina tarjuma za lugha mbali mbali, imesema taarifa ya wizara hiyo.

Msikiti wa Nimrah ulioko Arafat, Msikiti wa Mash’ar al-Haram ulioko Muzdalifah, Msikiti wa Al-Khaif huko Mina, na misikiti mingine kwenye njia ya Mahujaji pia imepokea Msahafu hiyo.

Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia inasema hatua hiyo inalenga kuwezesha Mahujaji kufaidika na ibada katika msimu huu wa Hija. Aidha Misahafu 80,000 mewekwa kwenye rafu kwenye Msikiti Mkuu wa Makkah.

Halikadhalika imedokezwa kuwa, Mahujaji mwaka huu watapata nakala ya Qur'ani Tukufu kama zawadi.

Mahujaji milioni moja wa Kiislamu kutoka nchi tofauti wamekusanyika Makka kwa ajili ya ibada ya Hija hii ikiwa ni mwara ya kwanza kupatikana idadi kubwa ya Mahujaji katika kipindi cha miaka miwili ya janga la Covid-19. Ibada ya Hija imeanza rasmi katika mji mtakatifu wa Makka leo Alhamisi.

4069194  

captcha