IQNA

Maoneyesho ya Qur'ani Tukufu

Tarjuma za Qur'ani Tukufu kwa lugha 76 katika Maonesho ya Vitabu ya Riyadh

19:00 - October 11, 2022
Habari ID: 3475915
TEHRAN (IQNA) – Tarjuma za Qur’ani Tukufu katika lugha 76 ni miongoni mwa vitabu vilivyoonyeshwa katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu yanayoendelea huko Riyadh, Saudi Arabia.

Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudia iliwasilisha tarjuma hizo, ambazo zimechapishwa na Kituo cha Uchapishaji Qur'ani cha Mfalme Fahd.

Wizara pia ilitoa zawadi ya nakala za Qur'ani na zenye tarjuma  kwa wageni tangu siku ya kwanza ya maonyesho ya vitabu yalipozinduliwa.

Kuonyesha filamu za matukio halisi, kutoa huduma za maktaba ya kielektroniki na kuwasilisha kazi za Kiislamu kuhusu masuala tofauti ni miongoni mwa shughuli nyingine za wizara hiyo katika hafla hiyo ya kitamaduni.

Kituo cha Uchapishaji Qur'ani cha Mfalme Fahd kiko katika mji mtakatifu wa Madina. Na huchapisha takribani nakala milioni 10 za Qur'ani Tukufu kila mwaka.

Pia huchapisha tarjuma na tafsiri za Qur'ani Tukufu katika lugha mbalimbali.

Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Riyadh 2022 yalizinduliwa katika mji mkuu wa Saudia tarehe 29 Septemba na yalimalizika tarehe 8 Oktoba.

Mashirika 1,200 hivi ya uchapishaji yanayowakilisha nchi 32 yalishiriki katika maonyesho hayo ya vitabu.

4090741

captcha