IQNA

Watu 40,000 watembelea Maonyesho ya Qur'ani Makka

14:55 - May 02, 2022
Habari ID: 3475196
TEHRAN (IQNA) – Zaidi ya watu 40,000 kutoka nchi mbali mbali duniani wametembelea Maonyesho ya Qur'ani Tukufu ambayo yamefanyika kaitka ukumbi wa Four Points wa Hoteli ya Sheraton Al Naseem katika mji mtakatifu wa Makka nchini Saudia.

Maonyesho hayo yameandaliwa na Idara ya Maonyesho na Makongamano kwa Ushirikiano na Taasisi wa Mfalme Fahd ya Kuchapisha Qur'ani.

Watliotembelea maonyesho hayo wameyasifu kutokana na uandalizi mzuri na manufaa tele yaliyomo.

Katika maonyesho hayo kuna picha zinazoelekeza historia ya Taasisi wa Mfalme Fahd ya Kuchapisha Qur'ani na taarifa zote kuhusu uchapishaji Qur'ani katika taasisi hiyo.  Aidha katika maonyesho hayo kuna tafsiri za Qur'ani kwa lugha mbali mbali ukiwemo Msahafu wa nukta nundu au braille.

3478746

captcha