IQNA

Diplomasia ya Kiislamu

Rais Raisi katika mkutano na Rais wa Sudan: Wazayuni ni chimbuko la masaibu mengi Afrika, duniani

19:42 - November 12, 2023
Habari ID: 3477884
RIYADH (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kuzungumza na Mkuu wa Baraza la Utawala wa Sudan na kuutaja utawala wa Kizayuni kuwa balaa kubwa kwa Umma wa Kiislamu na ulimwengu mzima.

Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Iran jana Jumamosi alikutana na Abdel Fattah al Burhan Mkuu wa Baraza la Utawala la Sudan pambizoni mwa kikao cha pamoja cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kilichofanyika mjini Riyadh Saudi Arabia na kutangaza kuwa Iran ipo tayari kubadilishana jumbe za kidiplomasia na kuimarisha uhusiano katika nyanja mbalimbali na Sudan. 

Katika mazungumzo hayo, Rais wa Iran ameutaja utawala wa Kizayuni kuwa balaa kubwa kwa Umma wa Kiislamu na ulimwengu mzima na akasema: utawala wa Kizayuni ndio chanzo cha masaibu mengi yanayoikabili dunia, chuki dhidi ya Uislamu, chuki dhidi ya Iran na mifarakano katika Ulimwengu wa Kiislamu na bara la Afrika.  

Kwa upande wake, Abdel Fattah al Burhan Kiongozi wa Baraza la Utawala la Sudan ameeleza kufurahishwa na fursa ya kukutana na kuzungumza na Rais Raisi na akasema: Sijaona kingine kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran isipokuwa kheri na wema na tuna hamu ya kujenga upya na kuanzisha tena uhusiano baina yetu." 

Mkuu wa Baraza la Utawala la Sudan amebainisha kuwa kuimarika kwa uhusiano baina ya nchi za Kiislamu zikiwemo Iran na Sudan ni kwa manufaa na maslaha ya Umma mzima wa Kiislamu na kwamba hii leo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndio nchi pekee inayoutetea waziwazi Uislamu. 

Raisi katika mazungumzo na Al-Sisi

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemwambia mwenzake wa Misri, Abel Fattal Al Sisi kwamba, matarajio ya jumla ni kwamba kivuko cha Rafah kifunguliwe ili misaada ya kimataifa iweze kuingia Ukanda wa Gaza.

Rais Ebrahim Raisi ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Rais wa Misri, Abed Fattah Al Sisi kandokando na mkutano wa viongozi wa nchi za Kiislamu na Kiarabu uliofanyika jana mjini Riyadh, Saudi Arabia, kujadili hali ya watu wanaoendelea kuuawa kwa mashambulizi ya Israel wa Ukanda wa Gaza.  

Sayyid Ebrahim Raisi ameongeza kwa kusema: Ni wazi kwa kila mtu kwamba Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel wanazuia kufunguliwa kivuko cha Rafah kwa ajili ya kupelekwa misaada ya kibinadamu kwa watu wanaodhulumiwa na wasio na ulinzi wa Gaza lakini vikwazo hivyo lazima viondolewe.

Raisi katika mazungumzo na Al-Sisi: Misri ifungue kivuko cha Rafah kwa ajili ya misaada kwa watu wa Gaza

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu Rais amekutaja kufanyika mkutano wa amani wa Cairo kuwa ulikuwa ubunifu mzuri ambao nchi za Magharibi zilizuia kufanikiwa kwake. Ameongeza kuwa: Mkutano wa amani wa Cairo ungeweza kuwa hatua muhimu ya kuhitimisha jinai zinazofanywa na Wazayuni katika mauaji ya wanawake na watoto wasio na ulinzi na wasio na hatia wa Gaza, lakini nchi za Magharibi zinazouunga mkono utawala wa Kizayuni, zimezuia mafanikio ya mkutano huo, kama ambavyo hazikuliruhusu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na na mashirika mengine ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti za kukomesha uhalifu huu.

Rais Ebrahim Raisi pia amesisitiza ulazima wa kuungana na kushikamana nchi za Kiislamu na kusema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haina kikwazo chochote katika kupanua uhusiano na nchi rafiki ya Misri. 

Kwa upande wake, Rais wa Misri, Abdel Fattah Al-Sisi, ameeleza kuwa Cairo ina irada ya uhakika ya kisiasa ya kuanzisha uhusiano halisi na Iran, na akasema: "Kwa sababu hiyo, tumewapa kazi mawaziri husika kuendeleza uhusiano wa kina baina ya nchi hizo mbili." 

4181214

Habari zinazohusiana
Kishikizo: Rais Raisi riyadh
captcha