IQNA

19:21 - January 26, 2022
Habari ID: 3474856
TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Qur'ani Tukufu kinachofungamana na Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Hadhrat Abbas AS nchini Iraq imezindua applikesheni mpya ya simu za mkononi ambayo inawasaidia wanafunzi kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

Apu hiyo hiyo ijulikanayo kama “Tarateel Alnoor” inatumia mfumo wa Android na inaweza kupatikana kupitia  Google Play. Unaweza kubonyeza hapa kuipata apu hiyo.

Afisa anayehusika na mradi huo, Bi Fatima al Sayyid Abbas Al Mousawi amesema apu hii ni moja ya apu kadhaa ambazo zimetayarishwa na kituo hicho cha Qur'ani kwa ajili ya kustawisha qiraa na ufahamu wa Qur'ani Tukufu.

Ameongeza kuwa apu hiyo imetengenezwa katika Kituo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano cha Al Kafeel.

Bi Fatima al Sayyid Abbas Al Mousawi amesema apu hiyo inatumia mbinu sahali ili kuwawezesha watumizi kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa njia rahisi.

4031410

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: