IQNA

Aplikesheni ya Kuhitimisha Qur'ani Tukufu yazinduliwa Kuwait

18:05 - May 14, 2022
Habari ID: 3475250
TEHRAN (IQNA)- Aplikesheni maalumu ambayo inawasiadia Waislamu kuhitimisha Qur'ani Tukufu imezinduliwa hivi karibuni nchini Kuwait.

Apu hiyo ambayo imepewa juna la "Qur'ani Sahbi' (Qurani ni Sahaba Wangu) imeundwa na Jumuiya ya Misaada ya Kuwait kwa ajili ya Huduma kwa Qur'ani Tukufu.

Tayari maelfu ya Waislamu wameshaanza kuitumia apu hiyo ili waweze kunufaika nayo. Afisa mwandamizi wa jumuiya hiyo Ahmed al Murshid amesema apu hiyo inmsaidia mtu kusoma Qur'ani binafsi, au pamoja na jamaa na marafiki.

Aidha inahesabu kila herufi  inayosomwa kama njia ya kukumbusha Hadithi ya Mtume Muhammad SAW isemayo kuwa kila anayesoma herufi katika Qur'ani  Tukufu, Allah SWT anampa thawabi 10.

Al Murshid anasema wanaotaka kuipata apu hiyo wanaweza kuipata kupitia majukwaa ya Google Play Store, Apple Store au katika tovuti ya hofath.org

4056806

Kishikizo: qurani tukufu ، aplikesheni ، apu ، kuwait
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :