IQNA

Darasa za kuhifadhi Qur’ani zinaendelea Gaza licha ya vikwazo

17:09 - December 10, 2025
Habari ID: 3481641
IQNA – Licha ya vizuizi vya utawala katili wa Israel na ukosefu wa vifaa, Wapalestina Gaza bado wana hamu ya kujifunza na kuhifadhi Qur’ani Tukufu, na wanashiriki katika vikao vya Qur’ani Tukufu.

Uharibifu wa kimfumo wa zaidi ya misikiti 1,100 wakati wa vita vya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza haujazima ari ya watu wa Gaza, wala haujapunguza shauku yao ya kujifunza Qur’ani.

Kituo cha Qur’ani cha Aisha kilichoko Gaza City kimeanza tena shughuli zake na kinaendesha madarasa ya hifdh na kozi za mafunzo kwa wanafunzi wa kiume na wa kike.

Mfanyakazi mmoja wa kituo hicho katika mazungumzo na Al Jazeera alisema kuwa, licha ya mabomu na kuuawa shahidi wakaazi wengi wa Gaza, wameendelea kusimama imara na hawajaondoka kaskazini mwa Gaza. Alisisitiza kuendeleza kazi yao kwa ajili ya wanafunzi na kwa radhi ya Mwenyezi Mungu, licha ya nafasi ndogo na ukosefu wa nakala za Qur’ani na vifaa, kutokana na utawala wa Kizayuni kuzuia kuingia kwa mahitaji muhimu wakati wa vita.

Mwalimu wa Qur’ani aliongeza: “Tunatarajia mtu atatusaidia kifedha, na kwa idhini ya Allah, itakuwa thawabu kwetu sote.”

Mwanaharakati wa Qur’ani alisisitiza kuwa licha ya hatari ya mashambulizi mitaani, yeye hutoka eneo la Sheikh Ajlain na hofu haijamzuia kuwahimiza wanafunzi kuhifadhi Qur’ani. “Mwenyezi Mungu ndiye mlinzi wetu na Yuko pamoja nasi,” alisema.

Sundus al-Khouli, mhifadhi wa Qur’ani kutoka Palestina, alieleza kuhusu kuvurugika kwa elimu na uharibifu wa misikiti na shule wakati wa vita, na akasema kuwa kituo hicho kilianzisha duruus ndogo za Qur’ani ili kufidia upungufu wa misikiti na shule.

Mwanafunzi huyo alisema kuwa licha ya ukubwa mdogo wa kituo na rasilimali chache, kimefanikiwa kuhitimu idadi ya wahifadhi wa kike ndani ya mwaka mmoja na nusu. Alisema kuwa alikabiliana na sauti za mabomu na uharibifu katika Ukanda wa Gaza na kwamba kituo kilifungwa mara kwa mara, lakini alianza kuhifadhi tangu utotoni na akafanikiwa kuhifadhi Qur’ani yote.

Alitoa mwito kwa Waislamu duniani kushikamana na Qur’ani na sala, akisisitiza kuwa ushindi unatoka kwa Mwenyezi Mungu na dini ndilo linalobaki maishani.

3495684

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu gaza
captcha