IQNA

Harakati ya PLO yatangaza kutoutambua utawala wa Israel

21:15 - February 10, 2022
Habari ID: 3474912
TEHRAN (IQNA)- Baraza Kuu la Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) imetangaza kusimamisha utambuzi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na ushirikiano wa kiusalama na utawala huo. Bunge Kuu la Palestina pia limetangaza kuwa, limesimamisha uratibu wowote wa kiusalama na utawala wa Kizayuni kwa njia mbalimbali.

Hatua ya PLO kusitisha utambuzi na kusimamisha ushirikiano wa kiusalama na Israel ina sababu kadhaa.

Jambo la kwanza ni kuhusiana na kushindwa kwa wazo la kushirikiana na utawala wa Kizayuni. Utambuzi wa utawala huo na ushirikiano nao ulikuwa na lengo la kuunda dola mbili za Palestina na Israel katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Kinachotokea leo ni kuwa, utawala wa Kizayuni hauamini juu ya kuundwa madola mawili na unaendelea kukalia kwa mabavu ardhi na kupora nyumba za Wapalestina kupitia ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni. Kuhusiana na suala hilo, Baraza Kuu la Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) lilitangaza katika taarifa yake kwamba limeamua kusitisha uamuzi kuutambua utawala wa Kizayuni na ahadi zote za Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuhusu mapatano yaliyofikiwa na Tel Aviv hadi pale taifa hilo litakapotambuliwa taifa la Palestina kwa msingi wa mpaka wa 1967.

 

Jambo la pili ni kuongezeka na kuenea jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina. Kwa upande mmoja jinai za Israel dhidi ya Wapalestina zimeongezeka, na kwa upande mwingine, huku huko nyuma jinai nyingi zikifanywa dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza.  Hivi leo pia watu wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, (Quds) Jerusalem na Ukanda wa Gaza wanashuhudia kwa wakati mmoja jinai za  utawala dhalimu wa Israel.

Kwa maneno mengine, jiografia ambayo utawala wa Kizayuni inafanya jinai dhidi ya Wapalestina imepanuka na kuwajumuisha Wapalestina wote. Katika uhalifu wa hivi punde zaidi, wanajeshi wa Israel walitekeleza hujuma ya kigaidi Jumanne iliyopita ambapo walifyatulia risasi gari la Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mji mjini Nablus katika eneo la Mukhfiya na kuwaua vijana watatu.

Jambo la tatu ni kwamba wananchi wa Palestina sasa wako mstari wa mbele katika kukabiliana na jinai zinazoongezeka za utawala haramu wa Israel unaoukalia kwa mabavu mji wa Quds na hata wametangulia Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika mapambano. Baada ya kuuawa shahidi vijana hao watatu katika mji Nablus, wakaazi wa Ukingo wa Magharibi waligoma na kufunga maduka na maduka yote. Kabla ya hapo wananchi wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quda waliungana na Wapalestina wenzao wa Ukanda wa Gaza katika vita vya siku 12 na utawala wa Kizayuni. Katika hali hiyo, kutochukua hatua yoyote ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina dhidi ya utawala wa Kizayuni ni sawa na kuukukbali utawala huo. Hivyo hatua ya sasa inachukuliwa katika fremu ya kuushinikiza utawala huo ghasibu.

Jambo la nne ni kukiri kwa wakuu wa utawala dhalimu wa Israel kwamba wanaendelea kuwaua Wapalestina na wanaona kuwa ni haki yao. Naibu Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel Elon Schuster alisema baada ya mauaji ya vijana watatu wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kuwa, "Utawala huo utahifadhi uhuru wake wa kuchukua hatua katika ardhi za Palestina kwa ajili ya kujilinda".

Waziri Mkuu wa utawala wa Israel Naftali Bennett na waziri wa vta wa utawala huo dhalimu Benny Gantz walipongeza mauaji ya kigaidi ya vijana watatu wa Kipalestina na kusisitiza kuwa "operesheni hizo zitaendelea katika siku zijazo." Kauli ya aina hii ya viongozi wa Israel ni kwamba kimsingi hawaamini katika ushirikiano wa kiusalama na Mamlaka ya Ndani ya Palestina, na wameitumia mamlaka  kama kikaragosi cha kufikia malengo na maslahi haramu ya utawala wa Kizayuni.

Muunganisho wa sababu hizo ulifanya Harakati ya Ukombozi wa Palestina, kusimamishwa kutambuliwa na kusitishwa ushirikiano wa kiusalama na utawala wa Kizayuni kwani hilo ni takwa la umma la watu na makundi ya Palestina kutoka kwa harakati hiyo.

6035828

Kishikizo: plo palestina israel
captcha