IQNA

Hamas yakosoa mkutano kuhusu uhusiano wa kawaida cha PLO na utawala haramu wa Israel

19:27 - August 07, 2021
Habari ID: 3474168
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani vikali kikao cha wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Harakati ya Ukombozi ya Palestina (PLO), mawaziri na maafisa wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na viongozi wa utawala haramu wa Israel chenye lengo la kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu.

Taarifa ya Hamas imeeleza kwamba, vikao kama hivi vinatilia alama ya swali thamani za kitaifa za Palestina na wakati huo huo vinajeruhi hisia za taifa la Palestina, wafungwa, mateka, majeruhi na familia za mashahidi wa Kipalestina.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo Hamas imesisitiza kuwa, hatua ya Harakati ya Ukombozi ya Palestina (PLO) na Mamlaka ya Ndani ya Palestina inakwamisha juhudi za taifa la Palestina na wanamapambano wake za kutetea na kupigania haki za wananchi madhulumu wa palestina mkabala na utawaa hramu wa Kizayuni wa Israel.

Kadhalika taarifa hiyo imeeleza kwamba, vikao kama hivi ni upotoshaji hatari na katu hatua kama hizi haziwezi kukubalika.

Hamas imeitaka mirengo, makundi yote ya Palestina pamoja na wananchi wa Palestina kwa ujumla kusimama na kukabiliana na hatua hizi za Harakati ya Ukombozi ya Palestina (PLO).

3988738

Kishikizo: hamas palestina plo
captcha