TEHRAN (IQNA)- Harakati za Kiislamu za kupigania ukombozi wa Palestina, Hamas na Jihad Islami zimesisitiza ulazima wa kuafikiana na Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) kuhusu mpango wa pamoja wa kitaifa wa kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel unaozikoloni ardhi za Palestina.
Habari ID: 3474978 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/26
TEHRAN (IQNA)- Baraza Kuu la Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) imetangaza kusimamisha utambuzi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na ushirikiano wa kiusalama na utawala huo. Bunge Kuu la Palestina pia limetangaza kuwa, limesimamisha uratibu wowote wa kiusalama na utawala wa Kizayuni kwa njia mbalimbali.
Habari ID: 3474912 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/10
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani vikali kikao cha wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Harakati ya Ukombozi ya Palestina (PLO), mawaziri na maafisa wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na viongozi wa utawala haramu wa Israel chenye lengo la kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu.
Habari ID: 3474168 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/08/07