IQNA

Mashindano ya Qur'ani, Hadithi ya Chuo Kikuu cha Al Mustafa ni makubwa zaidi duniani

19:13 - March 02, 2022
Habari ID: 3474996
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya ya kila mwaka ya Qur'ani Tukufu na Hadithi ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa ni tukio kubwa zaidi la Qur'ani Tukufu na Hadithi Duniani.

Hayo yamedokezwa na Hujjatul Islam wal Muslimin Muhammad Hussein Rafiei ambaye ameongeza kuwa mashindano hayo hulenga kuimarisha ufahamu wa Qur'ani Tukufu na Hadithi miongoni mwa wanachuo, waliohitimu na familia zao.

Hujjatul Islam wal Muslimin Rafiei ambaye pia ni mkuu wa Idara ya Qur'ani na Hadithi katiika chuo hicho amesema mashindanyo yam waka huu ambayo ni ya 27 yanamalizika Jumatano na kwamba washiriki wameshindana katika kategoria 27. Amesema miongoni mwa kategoria zilizokuwepo ni mashidano ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu, Adhana, Ibtihal na Qaswida.

Amesema mashindano hayo yalijumuisha washiriki 14,000 wanaofungamana na chuo hicho na kuongeza kuwa, mashindano pia yamefanyika katika matawi ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa katika nchi kama vile Afghanistan, Iraq, Uturuki, Russia, Turkmenistan, Indonesia, Thailand, Sri Lanka, Bangladesh, Madagascar, Niger, Nigeria, Tanzania na Pakistan.

4039707

captcha