Hujjatul Islam Ali Abbasi aliyasema hayo alipotembelewa chuo hapo na ujumbe wa Iraq kutoka Hauza au Seminari ya Kiislamu ya Najaf.
Amesema utawala wa Kizayuni wa Israe ni ngome ya ustaarabu wa kikoloni na kimaada wa Magharibi katika moyo wa ulimwengu wa Kiislamu.
Amelitaja suala la Palestina na utawala wa Kizayuni kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina kuwa ni suala la ustaarabu na kuongeza kuwa wakoloni wameuweka utawala bandia wa Kizayuni katika ulimwengu wa Kiislamu ili kulinda maslahi yao haramu.
Hujjatul Islam Abbasi aliashiria vita vya mauaji ya halaiki ya Israel katika Ukanda wa Gaza na kusema kile ambacho kimekuwa kikifanyika Palestina katika kipindi cha miezi saba iliyopita ni matokeo ya matukio yaliyoanza miongo kadhaa iliyopita na sasa yamegeuka kuwa makabiliano ya kistaarabu.
Kwingineko katika maelezo yake, alifafanua kuhusu shughuli za Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa, akisema ni kituo cha kitaaluma chenye utambulisho wa hauza au seminari ya Kiislamu.
Ameongeza kuwa, hivi sasa maelfu ya wanafunzi kutoka nchi 130 wanasoma sayansi ya Kiislamu na mafundisho ya Ahl-ul-Bayt (AS) katika chuo hicho.
Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa ni chuo kikuu cha kidini na Kiislamu kilichoanzishwa ili kupanua na kuanzisha mafundisho ya Kiislamu na kidini duniani kupitia vifaa na teknolojia za kisasa.
Ni taasisi ya kielimu na kielimu ambayo kama taasisi zingine kama hizo hujitahidi kukuza fikra na kusaidia jamii na ubinadamu.
Chuo hiki cha hadhi ya juu sasa kinajulikana kimataifa na kimetoa mafunzo kwa wasomi na watafiti wengi mashuhuri.
Aidha chuo hiki kina matawi mengi ya ng'ambo kwa Waislamu wasio Wairani wanaotaka kusoma Uislamu na masomo yanayohusiana nayo.
Chuo hiki hutoa shahda ya kwanza, shahada ya uzamili na pia shahada ya uzamivu au PhD.
3488364