IQNA

Rais wa Zanzibar aunga mkono shughuli za Chuo Kikuu cha Al Mustafa

13:39 - February 26, 2022
Habari ID: 3474976
TEHRAN (IQNA)-Rais wa Zanzibar amezitaja shughuli za kielimu na kimaarifa zinazofanywa na tawi la Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa kuwa ni muhimu na kutangaza kuunga chuo hicho katika shughuli zake eneo la Zanzibar nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa IQNA, Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ameyasema hayo, katika kikao na rais na maafisa wengine wa ngazi za juu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Mustafa nchini Tanzania, ambapo  amekaribisha na kutoa shukrani za dhati kutokana juhudi za chuo hiki cha kimataifa na kusema: "Ukuaji, ubora na ustawi wa kielimu  miongoni mwa watu wa Afrika, hususan eneo la Zanzibar, ni muhimu sana kwetu, na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa kimekuwa na mafanikio makubwa na yenye ufanisi katika mwelekeo huu, ambao unastahiki pongezi na shukurani."

Rais wa Zanzibar aliendelea kwa kusema: "Mtazamo wa viongozi na wapanga mipango wa Zanzibar kuhusiana na maendeleo ya kielimu katika eneo hili ni mkubwa na muhimu sana, hivyo tuko tayari kuendeleza maingiliano ya kielimu na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa."

Dkt.. Mwinyi aliashiria ripoti iliyowasilishwa na Hujjatul Islam wal-Muslimin Ali Taghavi, mkuu wa ofisi ya Mustafa nchini Tanzania, na kuongeza kuwa ana hamu ya kuona yaliyotajwa yanafikiwa kupitia ushirikiano wa karibu huku akisisistiza ulazima wa kufuatiliwa yaliyojadiliwa katika kikao hicho.

Rais wa Zanzibar alisema: "Kwa mara ya kwanza tunajenga mji wa kielimu na vyuo vikuu Zanzibar, na kwa kuzingatia nafasi ya kielimu na kisayansi ya Chuo Kikuu cha Al-Mustafa, ekari kadhaa zimetengwa katika eneo hilo kwa ajili ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa."

Akielezea kufurahishwa kwake na mkutano huu, Dkt. Mwinyi alisisitiza: "Ushirikiano wa kisayansi katika zama za sasa ni hitajio muhimu na la msingi ambalo linaweza kuongeza kiwango cha ufahamu wa umma kunaweza kuwa na athari na baraka kwa kizazi cha leo na cha baadaye, kwa hivyo mazungumzo yaliyofanyika na maamuzi yaliyochukuliwa nitayaelekeza kwa mawaziri husika ili tukio hatua hii muhimu ichukuliwe haraka iwezekanavyo.

Mwanzoni mwa mkutano huo, Hujjatul Islam wal Muslimin Ali Taghavi, Mkuu wa ofisi ya mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa aliwasilisha ripoti ya shughuli za kimataifa, kisayansi na kielimu za Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa.

حمایت رئیس جمهور زنگبار از فعالیت‌های علمی جامعةالمصطفی

4038703

captcha