IQNA

Elimu katika Uislamu

Vyuo vikuu vya Al Mustafa na Kampala vyatia mapatano ya kukuza uhusiano

16:58 - September 07, 2022
Habari ID: 3475746
TEHRAN (IQNA) – Wawakilishi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa na Chuo Kikuu cha Kampala cha Uganda wametia saini Mkataba wa Maelewano unaolenga kuboresha ushirikiano wa kielimu baina ya nchi hizo mbili.

Hati hiyo ilitiwa saini katika hafla mjini Kampala, Uganda, siku ya Jumanne na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa Hujjatul Islam Ali Abbasi na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala Profesa Badru D. Kateregga.

Kubadilishana maprofesa, kukuza ushirikiano wa pamoja wa kisayansi, na kuendeleza kozi za kujifunza mtandaoni ni miongoni mwa yaliyomo katika mapatano yaliyotiwa saini.

Akihutubia mkutano huo, Profesa Kateregga alibainisha kuwa Chuo Kikuu cha Kamapala kina kampasi tano ndani ya Uganda pamoja na vingine viwili nchini Kenya na Rwanda ambavyo vinapokea jumla ya wanafunzi 10,000.

Huku akiashiria historia ya uhusiano na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa na ubalozi wa Iran nchini Uganda kuhusu programu mbalimbali kama vile kufanya mashindano ya Qur'ani Tukufu na kuandaa kozi za lugha ya Kiajemi, profesa huyo alitarajia kwamba makubaliano mapya ya MoU yangefungua njia ya kuongezeka uhusiano kati ya pande hizo mbili.

Abbasi, kwa upande wake, aligusia sifa chache za Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa, akibainisha kuwa makumi ya maelfu ya wanafunzi kutoka nchi 130 wanasoma kozi katika matawi tofauti ya kituo hicho cha masomo.

Kulingana na yeye, chuo kikuu kimetia saini zaidi ya makubaliano 200 na vyuo vikuu kote ulimwenguni.

Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa ni chuo kikuu cha kidini na Kiislamu kilichoanzishwa ili kupanua na kutambulisha mafundisho sahihi ya Kiislamu na kidini kwa ulimwengu kupitia vifaa na teknolojia za kisasa.

Ni taasisi ya kielimu na kisayansi  ambayo kama taasisi zingine kama hizo hujitahidi kukuza fikra na kusaidia jamii na ubinadamu.

Inajulikana kimataifa na imefunza wasomi na watafiti wengi mashuhuri.

/3480375

captcha