IQNA

Mitandao ya intaneti ya Israel yashambuliwa katika hujuma kubwa zaidi

18:48 - March 15, 2022
Habari ID: 3475044
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mawasiliano wa utawala haramuIsrael, Yoaz Hendel, amekiri kuwa hitilafu iliyoathiri tovuti kadhaa rasmi ni matokeo ya shambulio la mtandao lililofanywa na wadukuzi, ambalo lililenga tovuti za utawala huo wa Kizayuni.

Awali vyombo vya habari vya Israel vilisema kwamba tovuti kadhaa za serikali, zilikabiliwa na hujuma kubwa na kuzima kutokana na mashambulizi ya mtandaoni.

Gazeti la Kizayuni la Haaretz limesema kuwa miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa ni tovuti za Wizara ya Mambo ya Ndani, Afya, Sheria na Ustawi na Ofisi ya Waziri Mkuu, Naftali Bennett.

Gazeti hilo lilinukuu chanzo cha usalama kikisema kuwa hilo ndilo shambulio kubwa zaidi la mtandao kuwahi kutokea dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel, na kwamba kuna uwezekano nchi au shirika kubwa limetekeleza hujuma hiyo.

Taasisi ya Ulinzi ya Kitaifa ya Mtandao wa Intaneti ya utawala haramu wa Israel imetangaza hali ya hatari ili kubaini ukubwa wa uharibifu huo, na kuchunguza athari zilizosababishwa na hujuma hiyo katika maeneo ya kimkakati na miundombinu ya serikali, kama vile makampuni ya umeme na maji.

Mashambulizi ya mtandaoni yamekuwa chaguo imara na la gharama ya chini kwa ajili ya vita na mashambulizi ya mtandao ya makundi mbalimbali dhidi ya miundombinu ya utawala wa Kizayuni; na kudukuliwa kwa taarifa muhimu na nyeti za utawala huo kumesambaratisha haiba bandia ya utawala huo katika masuala ya teknolojia ya mawasiliano. 

4042999

Kishikizo: israel mitandao
captcha