IQNA

Facebook yafuta ukurasa wa Televisheni ya Al Alam katika hujuma mapya ya uhuru wa kusema

17:21 - March 07, 2022
Habari ID: 3475020
TEHRAN (IQNA)- Kampuni kubwa ya mitandao ya kijamii ya Marekani ya Facebook imefuta "daima" ukurasa wa mtandao wa habari wa televisheni ya Iran wa al-Alam TV kwenye jukwaa lake bila kutoa notisi yoyote mapema.

Hujuma hiyo mpya dhidi ya uhuru wa kujieleza inakuja wakati ukurasa wa Facebook wa Televisheni ya al-Alam, ambao ulizinduliwa mwaka wa 2010, ulikuwa umevutia wafuasi 6,000,000 katika miaka iliyopita.

Awali Facebook ilikataa kusajili ukurasa wa al-Alam TV, ikidai kuwa mtandao huo wenye makao yake Tehran haukufuata masharti yake kuhusu uchapishaji wa picha za bendera na viongozi wa Hizbullah ya Lebanon, Ansarullah ya Yemen na makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina.

Hii ni wakati baadhi ya vyombo vingine vya habari vikichapisha kwa uhuru picha za viongozi wa makundi ya magaidi wakufurishaji, likiwemo kundi la kigaidi la al-Qaeda, kwenye kurasa zao za Facebook.

Ukurasa wa Facebook wa Televisheni ya al-Alam ulikuwa umezuiwa "kwa muda" mnamo Januari 2020 kufuatia mauaji ya kamanda mkuu wa kupambana na ugaidi wa Iran, Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na mwenzake wa Iraq Abu Mahdi al-Muhandis, naibu mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi katika hujuma  ya ndege zisizo na rubani za Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad.

Mwishoni wa mwa Januari mwaka huu, Facebook ilifuta kabisa ukurasa wa televisheni ya  lugha ya Kihispania ya Iran, Hispan TV.

Katika miaka iliyopita, Facebook - pamoja na YouTube, Twitter na Google - zimelenga mara kwa mara vyombo vya habari vya Iran na nchi zinazokosoa ubeberu wa madola ya Magharibi na na utawala wa Israel  unaokaliwa ardhi za Palestina kwa mabavu.

Januari iliyopita, Facebook ilizima kwa muda mfupi akaunti ya Press TV yenye wafuasi karibu milioni nne, kwa madai kwamba mtandao wa kimataifa wa habari wa Kiingereza wa Iran haukustahili kutumia jukwaa la mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, ilibatilisha uamuzi huo saa chache baadaye kutokana na rufaa iliyowasilishwa na Press TV.

4041048

captcha