IQNA

Msomi wa Kiitaliano aeleza ni kwa nini alianza kutafsiri Qur'ani

12:10 - April 25, 2022
Habari ID: 3475167
TEHRAN (IQNA) – Abdulwahab Ciccarello ametafsiri Qur'ani Tukufu kwa Kiitaliano na anasema msukumo wake ulikuwa kutoa tafsiri ambayo imezingatia mtazamo wa Kiislamu.

Kikao kwa njia ya intaneti ambacho kilipewa jina la "Masomo ya Qur'ani nchini Italia kwa mtazamo wa tafsiri ya Qur'ani ya Abdulwahab Ciccarello" hivi karibuni kiliandaliwa na Shirika la Habari la IQNA ili kujadili masomo ya kitaaluma ya Qur'ani katika nchi hiyo ya Ulaya.

Mohammad Taghi Amini, Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Italia, alikuwa mzungumzaji wa kwanza wa mtandao huo ambaye aliashiria shughuli za vyuo vikuu kadhaa vya Italia katika uwanja wa masomo ya Kiislamu.

Alielezea kazi ya Ciccarello kama mojawapo ya tafsiri sahihi zaidi za Kiitaliano za Qur'ani

Alizaliwa katika kijiji kidogo karibu na Venice mwaka wa 1965, Ciccarello alisoma fasihi ya Kiitaliano na kisha  alijifunza Kiarabu baada ya kuishi UAE kwa miaka kadhaa na kupitia safari zake za Saudi Arabia, Syria, na Tunisia.

“Nilifahamiana na walimu kadhaa waliofunza Kiarabu katika chuo kikuu na kupendezwa na lugha hiyo. Nilikuwa Mkristo wakati huo lakini nilisoma dini nyinginezo, hasa Uislamu, na hivyo nikavutiwa na Uislamu,” alisema na kuongeza kuwa alisilimu mwaka 1985.

Alipoulizwa kuhusu msukumo wake wa kutafsiri Quran, Ciccarello alisema “Kulikuwa na ongezeko la idadi ya Waitaliano waliokuwa wakiingia katika Uislamu katika miaka ya 1980 na hivyo kulikuwa na haja ya tafsiri ya Kiitaliano ya Quran. Kuna tafsiri nyingine  pia lakini nyingi zao zina mtazamo wa kikakademiki tu na wafasiri wao wengi wao si Waislamu. Tafsiri zao si zenye makosa bali zina maoni ya kilimwengu na ya kihistoria.”

"Kwa hiyo niliona kwamba kuna haja ya kutafsiri Qur'ani kwa mtazamo wa Kiislamu ili kuweka wazi kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni tofauti na ya mwanadamu yeyote."

Toleo la kwanza la tafsiri hiyo lilichapishwa mnamo 1993, alisema.

"Ingawa tafsiri ya Qur'ani iliisha miaka mingi iliyopita, bado napitia tafsiri ili kuiboresha."

"Tafsiri yangu ilikamilishwa kwa msaada wa kamati iliyojumuisha wataalamu wa lugha za Kiarabu na Kiitaliano pamoja na wanazuoni wa Kiislamu," alisema na kubainisha kuwa kamati hiyo ilianza kazi hiyo mwaka 1998 na tangu wakati huo matoleo kadhaa ya tafsiri hiyo yamechapishwa. ya mwisho mwaka 2021.

"Tulitumia tafsir zilizoandikwa na wanazuoni wa Sunni na Shia ili kuwa na ufahamu bora wa Qur'ani," Ciccarello alisema, akiongeza kuwa tafsiri hiyo inajaribu kutumia lugha ya kisasa ili wasomaji waweze kuelewa dhana kwa urahisi.

نشست مطالعات قرآنی آکادمیک در ایتالیا

رویکرد غیرسکولار و استفاده از زبان روز؛ ویژگی ترجمه جدید قرآن به زبان ایتالیایی

3478628

captcha