IQNA

Misikiti Italia haitafunguliwa wakati wa Idul Fitri

8:46 - May 14, 2020
Habari ID: 3472765
TEHRAN (IQNA) – Misikiti nchini Italia itaendelea kufungwa wakati wa Sala ya Idul Fitri ikiwa ni katika muendelezo wa kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.

Jumuiya ya Jamii za Waislamu Italia (UCOII) imesema hata kama serikali itaruhusu maeneo ya ibada yafunguliwe, Waislamu wamechukua uamuzi wa kuendelea kufunga maeneo yao ya Ibada kwa muda.

Misikiti, kumbi za sala na vituo vya Kiislamu ni kati ya maeneo ya ibada yaliyofungwa tokea Italia iweke zuio kw alengo la kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 nchini humo.

Makanisa ya Katoliki yametangaza mpango wa kuanza tena ibada kuanzi Mei 18 baada ya serikali kutangaza kufungua baadhi ya maeneo hatua kwa hatua.

Lakini pamoja na hayo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Jamii za Waislamu Italia (UCOII) Yassine Lafram amesema katika taarifa kuwa, misikiti ya Italia itaendelea kufungwa hadi baada ya Idul Fitri. Amesema viongozi wa Waislamu wameona ni busara kuendelea kufunga misikiti na kumbi za sala hadi baada ya Ramadhani na sherehe za Idul Fitri.

Aidha amesema wameshaweka kanuni za kiafya ambazo zitafuatwa wakati wa kufunguliwa tena misikiti ikiwa ni pamoja na waumini kuvaa maski, glavu na kuzingatia umbali baina yao wakati wakati wakiwa katika maeneo ya ibada. Aidha amesema maeneo yote ya Swala yatasafishwa mara kwa mara kwa dawa za kuua virusi na watu waumini watafuata utaratibu maalumu wa kuingia na kutoka katika maeneo ya ibada.

Itali ni kati ya nchi ambazo zimeathiriwa vibaya zaidi na ugonjwa wa COVID-19 duniani  ambapo hadi kufikia Mei 14 watu 222,000 walikuwa wameambukizwa ugonjwa huo nchini humo na miongoni mwao 31,106 wamefariki.

3471421

Kishikizo: italia waislamu COVID-19
captcha