IQNA

Fikra za Imam Khomeini

Irfani na Urazini katika Mawazo ya Imam Khomeini

16:17 - June 01, 2022
Habari ID: 3475323
TEHRAN (IQNA)- Ijapokuwa Imam Khomeini anajulikana kuwa kiongozi wa kimapinduzi na shakhsia wa kisiasa, alikuwa na shughuli na nadharia muhimu katika uga wa irfani (mysticism) na sayansi ya kidini. Aliarifisha irfani kama kama njia inayotokana na Qur'ani na Sunnah.

Mtazamo wa Imam Khomeini kuhusu irfani una sifa nne.

Kwanza kabisa, inatokana na Qur'ani Tukufu, Hadith, riwaya, na dua. Aliamini kuwa Qur'ani na Sunnah ni vyanzo vikubwa vya maarifa ya kinadharia na kivitendo ya irfani kwa namna ambayo Muislamu hapaswi kujiruhusu kutumia itikadi nyinginezo za irfani.

Sifa ya pili ni kwamba aaliunganisha irfani na ulimwengu. Irfani wakati mwingi imekuwa ikihusishwa na kujitenga na jamii lakini ingawa alikuwa mwana irafani, hakupuuza siasa na jamii na ndio sababu aliweza kuibua mapinduzi makubwa zaidi ya kisiasa. Alisema kwamba aliutazama ulimwengu kutoka kwa mtazamo wa irfani.

Sifa ya  tatu ni uhusiano wa irfani na urazini. Tatizo kubwa la wanairfani na wasomi wa wanazuoni lilikuwa imani kwamba kuna mgongano kati ya umaizi na hoja. Kuna njia za irfani ambazo zinapinga kabisa urazini. Hata hivyo, Imam Khomeini aliamini kwamba kuna maelewano kati ya urazini na irfani.

Sifa ya nne ni uhusiano wa irfani  kweli na upendo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, au kwa maneno mengine, uhusiano wa mapenzi na irfani. Mtu hawezi kweli kuelewa irfani ya Imam Khomeini bila ya kuisoma katika fremu ya upendo wa Mwenyezi Mungu.

Kwa mtazamo wa Imam Khomeini, Tauhidi ni nguzo ya irfani. Anasema kwamba irfani ya kimatendo ina nafasi kubwa zaidi katika irafani; Tauhidi ya vitendo ina maana ya kujua na kuamini kwamba kila kitu katika ulimwengu huu kinatawaliwa na Mwenyezi Mungu. Imam Khomeini aliamini kwamba tauhidi ya kivitendo inaweza kupelekea kuboreka mtu binafsi, kukataa ibada ya masanamu, kutotii maadui wa Mwenyezi Mungu, uboreshaji wa kijamii, matumaini yasiyo na mwisho, juhudi kubwa, subira, na hisia ya kujitolea zaidi.

Makala haya yalikuwa muhtasari wa hotuba iliyotolewa na Mohammad Beheshti, wa kitivo katika Taasisi ya Utafiti ya Seminari za Kiislamu na Vyuo Vikuu, katika warsha iliyofanyika Februari 2021.

Ayatullah Seyed Rouhollah Mousavi Khomeini (1902-1989), anayejulikana zaidi kama Imam Khomeini, alikuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na  Marjaa wa Kishia. Ameandika kazi mbalimbali za Fiqh, Falsafa ya Kiislamu na Irfani

3479134

captcha