IQNA

Sunnah za Mwenyezi Mungu katika Quran/2

Sunnah ya Istidraj

23:55 - August 24, 2024
Habari ID: 3479325
IQNA – Kwa maneno ya Qur’ani, Istidraj ni mojawapo ya Sunna za Mwenyezi Mungu zisizobadilika na zilizoenea.

Katika Sunnah hii, hatua kwa hatua mtu anavutwa kwenye shimo lisilo na mwisho na maangamizi kutokana na kutomtii Mwenyezi Mungu na kusisitiza juu ya kuendelea na dhambi.

Katika Istidraj, makundi kama hayo ya watu kama makafiri hupata adhabu ya Mwenyezi Mungu.

Watu wengi waliokataa wito wa manabii wao walikumbwa na Istidraj. Tofauti na baadhi ya adhabu za Mwenyezi Mungu zinazokuja kwa haraka, Istidraj hutokea hatua kwa hatua.

Suala la Istidraj limezungumziwa katika aya mbili za Quran:

Aya ya 182 ya Suratul-A’raf: “Na wale walio kadhibisha Ishara zetu, tutawapururia pole pole kwa namna ambayo wenyewe hawaijui.”

Aya ya 44 ya Surah Al-Qalam: “Basi niache na wanao kadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kwa mahali wasipo pajua.”

Aya hizi zinaeleza jinsi mtu, baada ya kuzikataa Aya za Mwenyezi Mungu, anaanguka katika mtego wa Istidraj na kuvutwa katika dhambi kidogo kidogo hadi kutoweka matumaini ya wokovu wake.

Mtazama wa Qur’ani Tukufu juu ya Istidraj unahusu kuondoka taratibu kutoka katika njia ya Mwenyezi Mungu kama matokeo ya kumsahau Yeye. Wale wanaoukataa uwongofu wa Mwenyezi Mungu na kushindwa mara kwa mara katika mitihani ya Mwenyezi Mungu hatimaye huachwa peke yao, na hata njia imeandaliwa kwa ajili ya kuanguka kwao, ili waweze kuukaribia mwisho wao mbaya na kupata adhabu ya Mwenyezi Mungu.

Sunnah ya Istidraj ina dalili fulani. Kwa mfano, haitumiki wakati wa shida na masaibu, lakini hujitokeza katika jamii wakati wa baraka na furaha.

Dalili ya adhabu inayotokana na Sunnah ya Istidraj ni kwamba wakati mtu huyo yuko katika hali nzuri za kidunia, anamsahau kabisa Mungu na hakuna dalili yoyote ya kiroho na uadilifu katika maisha yake. Kwa hivyo ikiwa mtu ana mali ya dunia na hali nzuri katika maisha na akazitumia neema hizi kwenye njia ya Mwenyezi Mungu, hii haitakuwa Sunna ya Istidraj.

3489586

Kishikizo: sunnah qurani tukufu
captcha