IQNA

Waziri wa zamani wa mambo ya nje Iran asema

Imam Khomeini alihuisha ujumbe wa Uislamu

14:39 - February 08, 2022
Habari ID: 3474905
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Iran amesema hayati Imam Khomeini- Mwenyezi Mungu Amrehemu, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alihuisha Uislamu na kuwapa Waislamu utambulisho

Manouchehr Mottaki ameyasema haya leo Jumanne mjini Tehran wakati akihutubu katika kongamano la kimataifa la “Mazungumzo ya Mapinduzi ya Kiislamu; Mbinu ya Mapambano (Muqawama) Duniani.”

Kongamano hilo limeandaliwa na Shirika la Habari za Qur'ani Tukufu la Kimataifa (IQNA) kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa 43 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Mottaki amesema ujumbe wa Mapinduzi ya Kiislamu ni sawa na ule wa Mtume Muhammad SAW nao ni kubadilisha mtazamo wa mwanadamu kuhusu dunia.

Huku akiashiria aya ya 38 ya Sura Ad Dukhan isemayo,” Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake kwa mchezo,” amesisitiza kuwa, kuumbwa dunia kuna falsafa na lengo ambalo limebainishwa katika aya ya 18 ya Sura al Anbiya isemayo: “Bali tunaitupa kweli juu ya uwongo ikauvunja na mara ukatoweka. Na ole wenu kwa mnayo yazua.”

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Iran amesema maisha ni medani ya mapambano ya daima na kukabiliana na uwongo. Ameendelea kusema kuwa Imam Khomeini alikuja kuhuisha mapambano hayo. Aidha Mottaki amesema Imam Khomeini alikuja na ujumbe mpya wa kuasisi ustaarabu mpya.

4034804

captcha