IQNA

Ugaidi wa wakufurushaji

Magaidi wa ISIS watekeleza hujuma dhidi ya Waislamu wa Kishia nchini Afghanistan

21:37 - August 06, 2022
Habari ID: 3475585
TEHRAN (IQNA)- Kundi la kigaidi la Daesh au kwa jina jingine ISIS, limekiri kuhusika na mlipuko uliotokea jana Ijumaa huko Kabul, mji mkuu wa Afghanistan, ambao ulipelekea watu 8 kuuawa shahidi na wengine 18 kujeruhiwa.

Tangu takriban mwaka mmoja uliopita tokea kundi la Taliban lirejee madarakani nchini Afghanistan, kundi la kigaidi la Daesh limefanya mashambulizi na milipuko mingi ya kigaidi katika nchi hiyo, ikiwemo milipuko mikubwa ya umwagaji damu iliyotokea katika mikoa ya Kunduz na Balkh. Hii ni licha ya kwamba Taliban daima imekuwa ikidai kuangamiza au kulidhoofisha pakubwa kundi hilo. Kwa kuzingatia hilo, mlipuko wa Ijumaa huko Kabul unaweza kutathmiiwa katika mitazamo miwili.

Mtazamo wa kwanza ni kuwa kundi la kigaidi la Daesh linatunisha misuli na kudhihirisha nguvu zake mkabala wa hatua za kiusalama za Taliban ili kuthibitisha udhaifu wake mbele ya kundi hilo na pili ni kwamba katika kukaribia siku za maombolezo za Tasua na Ashura  ya Imam Hussein AS, ambapo Taliban imechukua hatua kali za kiusalama, mlipuko huo wa kigaidi, unaibua dhana kwamba huo ni utangulizi wa Taliban kutekeleza siasa kali dhidi ya maombolezo ya kuuawa Shahidi Imam Hussein AS na wafuasi wake wachache waaminifu.

/3479987

Kishikizo: afghanistan ، isis au daesh ، taliban
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha