IQNA

Qur’ani Tukufu Inasemaje/9

Je, Unamjua Adui Yako?

21:49 - October 17, 2022
Habari ID: 3475946
TEHRAN (IQNA) – Baada ya Mwenyezi Mungu kumuumba mwanadamu, kuna Yule mwenye kiburi aliyeaanza uadui dhidi yake.

Mwenyezi Mungu alipomuumba mwanadamu na kupuliza roho yake ndani yake, mwanadamu huyo alitajwa kuwa ndiye kiumbe bora zaidi kwani angeweza kufikia ukamilifu na wema ambao hakuna kiumbe mwingine angeweza kufikia. Mungu aliwataka malaika wote wamsujudie Adam. Shetani hakufanya hivyo kwa vile aliamini kuwa yeye ni mkuu kuliko mwanadamu. Kisha Mwenyezi Mungu akamkataa na kumtaka atoke nje ya bustani.

Hii ndiyo sababu Shetani amekuwa adui wa mwanadamu na ameapa kumpotosha mwanadamu kutoka kwenye njia ya ukamilifu. “Akasema (Iblisi): Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote (wanaadamu), (Surah Sad, Aya ya 82).

Kisa hiki  pia kimetajwa katika aya ya 34 hadi 39 ya Sura Baqarah.

Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, Shetani anaweza kumpotosha mwanadamu kutoka kwenye njia ya Mungu kwa kumshawishi kufanya dhambi.

Mwenyezi Mungu amemtaja Shetani kuwa ni adui wa mwanadamu mara kadhaa ndani ya Quran, ikiwa ni pamoja na “Wala asikuzuilieni Shetani. Hakika yeye ni adui yenu wa dhaahiri.” (Sura Az-Zukhruf, aya ya 62).

Mwalimu na mtafiti wa Qur’ani Tukufu Hujjatul Islam Mohsen Qaraati anaashiria jumbe mbili za aya hii:

- Kwa kuzingatia historia ya Shetani kuwadanganya Adamu na Hawa, uadui wake ni dhahiri kwa kila mtu.

- Kuelewa majaribu ya Shetani hakuhitaji tafakari ya ziada kwani mwanadamu anaelewa kupotoka kwa kawaida.

Sasa, ni nini umuhimu wa kuelewa uadui wa Shetani kwa wanadamu? Ikiwa tunakubali kwamba mwanadamu ana mwelekeo wa kustawi na kufikia ukamilifu kupitia mwongozo, basi anahitaji kujua vizuizi vilivyo kwenye njia hii. Kwa hiyo, mojawapo ya kazi kuu za kila mwanadamu ni kumtambua adui huyu na mbinu anazotumia Shetani kumshawishi.

captcha