IQNA

Qur'ani Tukufu Inasemaje /40

Hadhi ya Manabii wa Mwenyezi Mungu; Kupokea Wahyi na kuongoza jamii

20:43 - December 12, 2022
Habari ID: 3476236
TEHRAN (IQNA) – Kuna nafasi tatu ambazo kila Mtume wa Mwenyezi Mungu amepewa angalau moja kati ya hizo na utume unaotokana na nafasi hiyo.

Miongoni mwa mitume wa Mwenyezi Mungu, Nabii Ibrahim (AS) ana hadhi na nafasi maalum. Jina lake limetajwa mara 69 katika Sura 25 za Qur'ani Tukufu. Kama Mtume Muhammad (SAW), ametambulishwa kama mfano wa kuigwa kwa wanadamu. Kwa kutumia busara, alipigana dhidi ya upotofu na Shirki katika nyanja tofauti. Alipewa hadhi ya Uimamu baada ya kufaulu mitihani mikubwa ya kiungu.

“Na Mola wake Mlezi alipo mjaribu Ibrahim kwa kumpa amri fulani, naye akazitimiza, akamwambia: Hakika Mimi nitakufanya uwe mwongozi wa watu. Akasema: Je, na katika vizazi vyangu pia? Akasema: Ahadi yangu haitawafikia wenye kudhulumu. 

Kwa uchache sehemu mbili za aya huu ni muhimu. Sehemu ya kwanza inayorejelea Uimamu wa Ibrahim (AS), na ya pili ambayo Mwenyezi Mungu anasisitiza usahaba wa kudumu wa Uimamu na uadilifu. Lakini nini maana ya Uimamu katika aya hii na inahusiana vipi na utume?

Ama kuhusu swali la kwanza, inapasa kusemwa kwamba baada ya kupita mitihani ya Mwenyezi Mungu, kila Mtume wa Mwenyezi Mungu amefikia baadhi ya hadhi, mojawapo ikiwa ni Uimamu.

Kulingana na Tafsiri ya Nemuneh ya Qur'ani Tukufu, utume ni nafasi ya mtu anayepokea ufunuo au Wahyi kutoka kwa Mwenyezi  Mungu. Kwa hiyo nabii ni yule ambaye Mwenyezi Mungu humpelekea ufunuo wake. “Risala” ni nafasi nyingine ambayo mtume amepewa jukumu la kufikisha na kueneza Wahyi na kukuza kanuni za Mwenyezi Mungu, hivyo kuelimisha na kuongeza ufahamu katika jamii. "Rasul" ni yule ambaye amepewa jukumu la kujitahidi kuunda mapinduzi ya kitamaduni na kiitikadi kwa mujibu wa kanuni za Mwenyezi Mungu.

Hadhi ya Uimamu, wakati huo huo, ina maana ya uongozi na utawala. Kwa hakika, Imamu ni yule anayesimamisha serikali ya Mwenyezi Mungu ili kutekeleza kanuni za Mwenyezi Mungu. Kwa maneno mengine, jukumu la Imam ni kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu na jukumu la Mtume ni kuanzisha tu na kufundisha amri hizo.

Kwa hiyo Uimamu ni hadhi ya juu na bora kuliko Utume na Risala, kwa sababu inahitaji sifa na fadhila kubwa katika maeneo mbalimbali. Ibrahim (AS) alipata hadhi hii baada ya kufaulu mitihani ya Mwenyezi Mungu na, kwa mujibu wa Quran Tukufu, hii ilikuwa hatua ya mwisho katika harakati zake za kuelekea kwenye ukamilifu.

Ujumbe wa sehemu ya kwanza ya aya ya 124 ya Surah Al-Baqarah, kwa mujibu wa Tafsiri ya Nemuneh ya Qur'ani Tukufu ni:

  • Hata Manabii wa Mwenyezi Mungu wanajaribiwa na Mwenyezi Mungu Mwenyewe. "Na Mola wake Mlezi alipomjaribu Ibrahim kwa maneno."
  • Ili kumteua mtu kwenye nafasi, kunahitajika kupimwa (kuthibitisha sifa). "Na Mola wake Mlezi alipomjaribu Ibrahim kwa maneno."
  • Vyeo vipewe watu taratibu na baada ya mafanikio katika kila hatua. "Alitimiza."
  • Uimamu ni hadhi anayopewa mtu kwa kuteuliwa (na Mwenyezi Mungu) sio kwa kupiga kura. Imamu lazima ateuliwe na Mwenyezi Mungu. “Hakika mimi nitakufanya Imamu.”
Habari zinazohusiana
captcha