IQNA

Qur'ani Tukufu Inasemaje / 13

Umuhimu wa Ayatul Kursi

14:19 - June 30, 2022
Habari ID: 3475444
TEHRAN (IQNA) – Aya ya Qur’ani Tukufu inayojulikana kwa jina la Ayatul Kursi ina umuhimu na fadhila maalum kutokana na mafundisho yake muhimu.

Ayatul Kursi inajulikana sana na ni mashuhuri miongoni mwa Waislamu. Kuna Hadith iliyopokelewa kutoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad  (SAW) inayoeleza aya ya 255 ya Surah Al-Baqara kama aya muhimu na tukufu zaidi katika Kitabu Kitukufu. Aya hii inajulikana kwa jina la Ayatul Kursi tangu mwanzo na Mtukufu Mtume (SAW) amelitaja jina hili katika Hadith.

Umuhimu maalum unaohusishwa na aya hii ni kwa sababu ya mafundisho matukufu iliyomo, ikiwa ni pamoja na maneno “Allah! Hakuna mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila Yeye, "ambayo inaashiria itikadi takasifu ya Tauhidi au Mungu Mmoja. Aya kamili ya Kursi ni kama ifuatavyo:

"Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu.

Majina ya Mungu na sifa zake yametajwa katika aya hii mara 16. Ndiyo maana Ayatul Kursi inatajwa kuwa ni kauli mbiu na ujumbe wa Tauhidi. La Ilaha Illa Allah (Hakuna Mola ila Allah) ni utambulisho wa kila Muislamu na kauli mbiu ya kwanza na mwaliko wa Mtukufu Mtume (SAW). Kuiamini ni chanzo cha wokovu kwa kila mwanadamu. Imani juu ya Tauhidi humfanya mtu achukue mamlaka na vivutio vyote kuwa havina umuhimu. Mfano wa mafunzo ya Tauhidi ni kwamba Waislamu walikuwa hawasujudu mbele ya wafalme, majabari na wenye nguvu.

Neno Kuishi Milele linamaanisha kwamba kifo na kutokuwepo hakuna maana tunapozungumza kuhusu sifa za Mwenyezi Mungu. Msimamoa mambo yote kunamaanisha kuwa dunia nzima inamtegemea Mwnyezi Mungu. Ukweli kwamba hata usingizi wala kulala hakumfikii, ina maana kwamba umakini Wake kwa ulimwengu hauna mwisho. Na Anamiliki kila kilichomo. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi.

Bila ruhusa au idhini  Yake, hakuna aliye na uwezo wa kuombea, ambayo ni msisitizo mwingine juu ya umoja wa Mwenyezi Mungu katika nguvu na mapenzi. Kwa hiyo, aya hii inakanusha sanamu au chombo chochote kinachotumiwa kudhoofisha utawala wa Mungu.

Neno Kursi (kiti) halipaswi kutazamwa kama kitu kinachoweza kuguswa au na kiti ambacho Mungu amekalia lakini, kama mfaisis mashuhuru wa Qur'ani Tukufu Allamah Tabatabai anavyobaini, Kursi ni daraja katika daraja za elimu ya Mwenyezi  Mungu ambayo hakuna mtu anayeweza kupima. Inaashiria uwezo wa Mungu na utawala wake juu ya mbingu na ardhi. Maneno "Yeye "anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao" pia yanarejelea ujuzi wa Mwenyezi Mungu usio na kikomo juu ya sasa na yajayo. Inaashiria kwamba vitu vyote ulimwenguni na ujuzi wote huo wa vilivyo katika mbingu na ardhi ni ujuzi wa Mwenyezi Mungu na ndio umeitwa Kursi.

Habari zinazohusiana
captcha