IQNA

Qur'ani Tukufu Inasemaje /33

Wito wa Mwenyezi Mungu wa Kujenga Umoja, Kuepuka Mgawanyiko

14:33 - November 07, 2022
Habari ID: 3476048
TEHRAN (IQNA) – Aya ya 130 ya Sura Aal Imran inauchukulia umoja baina ya Waislamu kuwa ni jambo la wajibu na inasisitiza kwamba Qur’ani Tukufu ndicho chanzo muhimu zaidi cha umoja katika Umma wa Kiislamu.

Mwenyezi Mungu ametuwekea fadhila kuu ambazo ziko juu zaidi ya rangi ya mtu, kaumu au kabila, mali n.k. Hizi ni fadhila ambazo  zinaweza kutuunganisha pamoja nazo ni ubinadamu, kufuata kanuni za Uislamu, na kukiri Upweke wa Mungu yaani kuwa na itikadi ya Tauhidi.

Umma wa Kiislamu hivi sasa unakabiliwa na tatizo kubwa na maadui wa Uislamu wanajaribu kudhoofisha umoja wa Waislamu kwa kubuni njama tofauti zenye za kidini, kilugha, kikabila na hata za kihistoria.

Chini ya hali hii nyeti, ni muhimu kwa Waislamu kutambua njama za maadui na pia njia za kuanzisha umoja na kujiepusha na kuibua migawanyiko.

Umoja huu ni muhimu sana kiasi kwamba Qur'ani Tukufu ina zaidi ya aya 50 kuhusu mada hii na sababu za mgawanyiko.

 “ Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka.” (Surah Al Imran, aya ya 103)

Aya hiyo inawaalika waumini kwenye umoja na inabainisha kwamba umma wa Kiislamu unapaswa kudumisha umoja kwa kushikamana na Tauhidi: hii ni sehemu ya Tauhidi ya kivitendo.

Aya hiyo pia inaashiria uadui uliopo baina ya watu kabla ya Uislamu, ikiwakumbusha athari za muujiza ya dini katika kuwaleta pamoja.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaalika watu wote, si Waislamu tu, kukusanyika kwa misingi ya ukweli na kuachana na migogoro na migawanyiko.

Tukitafakari kwa undani zaidi aya za Qur'ani, mtu anaweza kutambua kwamba kuepuka mgawanyiko ni mojawapo ya kanuni za kimsingi za miito ya Mwenyezi Mungu.

Pia kuna tafsiri tofauti kuhusu " Kamba ya Mwenyezi Mungu " ambayo imetajwa katika aya. Baadhi ya wataalamu wanaamini inarejelea Qur'ani Tukufu  yenyewe na wengine wanasema inaelekeza kwenye Qur'an, Sunna, dini ya Mwenyezi Mungu, kumtii Mwenyezi Mungu, Tauhidi kamili, na Wilaya au Mamlaka ya ya Ahlul-Bayt (SA) yaani watu wa nyumba ya Mtume Muhammad SAW..

Kwa mujibu wa amri zilizotajwa katika Qur'ani Tukufu na Sunnah za Mtume Muhammad (SAW), ikiwa Waislamu wanataka kuwa na nguvu, wanapaswa kusisitiza umoja na kulinda kanuni na maadili yanayotokana nao.

Ndiyo maana mbinu kadhaa zimependekezwa ili kuunda na kudumisha umoja ikiwa ni pamoja na, kurejelea Qur'an na Sunnah ili kutatua tofauti, kuzingatia matendo yanayohusiana na umoja, kuimarisha uhusiano, kuunda mazingira ya mazungumzo, na kuzingatia wajibu wa maadili.

Qur'ani inatufundisha kwamba kama kundi la watu haliko tayari kushirikiana nawe katika malengo yote ya Mwenyezi Mungu, unapaswa kujaribu kuwavutia ili upate urafiki wao kwa ajili ya kufikia malengo makuu ya pamoja.

Habari zinazohusiana
captcha