IQNA

Qur'ani Tukufu Inasemaje /37

‘Kumkopesha Mwenyezi Mungu’: Uhimizo wa Qur’an wa Kuwasaidia Wenye Mahitaji

19:09 - November 22, 2022
Habari ID: 3476129
TEHRAN (IQNA) – Ibara ya “kumkopesha Mwenyezi Mungu” imetajwa mara saba ndani ya Qur’an Tukufu kama uhimizaji dhahiri wa kuwasaidia wenye shida. Kifungu hiki cha maneno kina maana fulani iliyofichwa.

 Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema ili amzidishie mzidisho mwingi, na Mwenyezi Mungu hukunja na hukunjua. Na Kwake Yeye mtarejea.” (Surah Baqarah, aya ya 245)

Kumkopesha Mwenyezi Mungu kunamaanisha kuwasaidia wale walio na uhitaji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Aya hapo juu inawakumbusha watu kwamba kuwasaidia wengine hakutasababisha kupungua kwa mali zao.

Suala la kumkopesha Mwenyezi Mungu limetajwa mara saba ndani ya Qur'ani Tukufu. Tafsir Majma‘ al-Bayan inataja baadhi ya masharti ya ukopeshaji huu, ikiwa ni pamoja na kwamba kiasi kinachopatikana kutoka kwa chanzo cha halali, kinatolewa bila ya kuutazama upande mwingine, kinatolewa kwa siri, na kinatolewa haraka huku kukilinda uso wa wahitaji.

Neno "Qardh" kwa Kiarabu linamaanisha aina ya kukata; kutumia neno hili inahusu ukweli kwamba sehemu ya mali ya mtu hukatwa na kupewa mtu mwingine na kisha kurudi.

Ibara ya Qur'ani Tukufu kuhusu "kumkopesha Mungu" inaonyesha kwamba malipo ya "Qardh al-hasan" (mkopo usio na riba) yatatolewa na Mwenyezi Mungu. Badala ya kuwaamuru waumini wawakopeshe wenye shida, Qur'ani Tukufu inawahimiza wamkopeshe Mwenyezi Mungu ili kuwatia moyo kufanya hivyo. Kwa upande mwingine, kifungu hiki cha maneno kinajaribu kukabiliana na hisia zozote za udhaifu kwa wahitaji kadri Mungu anavyojiweka katika viatu vyao.

Kwa kuwa wanadamu wanatafuta masilahi, aya hiyo inajaribu kuwatia moyo, ikisema kwamba mkopo huo utarejeshwa "kwa fungu nyingi".

Malipo ambayo Mwenyezi Mungu hulipa wakopeshaji ni duniani na akhera.

Ujumbe wa Aya kwa mujibu wa Tafsir Noor

  • Kuwasaidia watu ni sawa na kumsaidia Mwenyezi Mungu
  • Watu wanahitaji kutiwa moyo kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji
  • Ikiwa tunaamini kwamba Mwenyezi Mungu "hupunguza na kuongeza vitu", tutatoa vitu vyetu kwa urahisi
  • Tukijua kuwa tutalipwa kile tulichotoa na tutarejea kwa Mwenyezi Mungu, tutatoa vitu vyetu kwa urahisi.
Habari zinazohusiana
captcha