IQNA

Qur'ani Tukufu inasemaje/19

Ghadir; Ujumbe wenye umuhimu sawa na Utume wa Mtume

15:16 - October 19, 2022
Habari ID: 3475954
TEHRAN (IQNA) – Akirejea kutoka katika Hijja yake ya mwisho, Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) alipokea aya kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambazo zilifungamanisha kukamilika kwa jumbe zote za Mwenyezi Mungu na ujumbe mmoja maalum.

Ujumbe huo, ambao kiini chake kilikuwa kuhusu Wilayat au uongozi wa Imam Ali (AS), ulifikishwa kwa watu katika eneo linalojulikana kama Ghadir Khumm.

Mtume Muhammad (SAW) alitekeleza Hijja yake ya mwisho, inayojulikana kama Hajjat-ul-Wida au Hajj ya kuaga, mwaka 632. Katika hija hii, alifuatana na Waislamu wapatao 120,000.

Baada ya kurejea Madina, yeye na wale waliofuatana naye walifika Ghadir Khum siku ya Alhamisi, tarehe 18 Dhul Hajja. Mara tu walipofika hapo, Aya iliteremshwa na Mwenyezi Mungu kwenye moyo wa Mtukufu Mtume (SAW):

" Ewe Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri." (Surah Al-Ma’idah, aya ya 67)

Ikiwa tutazingatia yaliyomo katika aya hii, tutagundua jinsi ilivyo muhimu. Inasema juhudi zote alizofanya Mtukufu Mtume (SAW) kwa zaidi ya miaka 23 tangu kuanza kwa wahyi zinakamilika kwa ujumbe maalum. Bila hivyo, ujumbe wote uliowasilishwa hadi sasa hautakuwa kamili.

Kwa amri ya Mwenyezi Mungu, Mtukufu Mtume (SAW) aliamuru kwamba kundi la Waislamu 120,000 lisimame na kukusanyika hapo.

Kwa kuzingatia idadi kubwa ya Waislamu waliokusanyika Ghadir Khum siku hiyo, ujumbe huo umeandikwa kwa usahihi na wafasiri wa Qur'an Tukufu , wasimulizi wa Hadith, na wanahistoria wameuhusisha na Tukio la Ghadir kwa yakini.

Mwanachuoni mkubwa na mwandishi wa juzuu 11 Al-Ghadir Allamah Amini (1902-1970) amesimulia tukio hili kutoka katika vyanzo 30 vya Hadith za Kisunni na tafsiri ya Quran.

Lakini ujumbe wa Ghadir ulikuwa upi?

Baada ya watu wote kukusanyika hapo, Mtukufu Mtume (SAW) aliongoza sala ya adhuhuri na kisha akaamuru matandiko ya ngamia yarundikwe kama mimbari ya muda juu ya kilima kidogo cha mchanga kilichoinuka. Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa Aalihi wa Sallam-Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake na Watu wa Nyumba Yake-) alifika hapo akatoa khutba: “Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema na Mjuzi "...Inaonekana wakati umewadia wa mimi kuitwa (na Mwenyezi Mungu) na hakika nitajibu wito huo. Ninawachieni vitu viwili vya thamani na kama mtakamatana navyo vyote viwili, hamtaweza kupotea baada yangu, navyo ni kitabu cha Mwenyezi Mungu na Watu wa nyumba yangu, yaani, Ahlul Bayt wangu. Viwili hivyo havitatengana mpaka vije kwangu peponi.”

Kisha mtume wa Mwenyezi mungu akaendelea: “Je, mimi sina haki zaidi juu ya waumini kuliko haki walizonazo juu yao wenyewe?”Waislamu walijibu wote kwa pamoja”Ndiyo bila shaka, Ewe ‘Mtume wa Mungu”

Kisha ikafuatiwa na sentensi muhimu iliyobainisha wazi wazi uteuzi wa Ali kuwa kiongozi wa Ummah wa Kiislamu. Mtukufu Mtume (saww) aliunyanyua juu mkono wa Ali bin Abi Talib a.s na kusema: “Kwa yeyote ambaye mimi ni Kiongozi wake (mawla), basi Ali ni Kiongozi wake (mawla).”

Kisha Mtume SAW akaendelea; “Eeh ‘Mwenyezi Mungu, wapende wale wanaompenda, na wachukie wale wanaomchukia.”].

Hizi ndio sehemu muhimu za hotuba ya Mtume. Pia kuna matoleo ya kina zaidi ya hutoba hii muhimu ya mtume ambayo yameandikwa na wanazuoni wengi wa kisunni.

Punde, kabla ya umati kutawanyika, Malaika Jibril (Jibril) alishuka tena na aya ya 3 ya Surah Al-Ma’idah katika Qur'ani Tukufu…

 “Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni uislamu uwe ndiyo Dini.

captcha