Kukataa au kuficha ukweli kumekuwa mojawapo ya mambo muhimu ambayo yamepotosha watu na jamii. Hili limeathiri umma wa Kiislamu tangu Uislamu wa mwanzo na hii ndio maana linazingatiwa miongoni mwa madhambi makubwa.
Kwa mfano, baadhi ya wanachuoni wa Kiyahudi waliozijua dalili za Mtume Muhammad (SAW) na walikuja Madina kumuona Mtume wa mwisho aliyetajwa kwenye Taurati, walijiepusha kumwamini kwa vile waliona kwamba wangepoteza maisha yao na nafasi za kidunia. Hawakusema ukweli na badala yake wakawa maadui wa Mtume Muhammad SAW. Hapo ndipo ilipoteremka Aya ya 159 ya Sura Baqarah: " Hakika wale wanao ficha tuliyo yateremsha nazo ni hoja zilizo wazi na uwongofu baada ya Sisi kuzibainisha kwa watu Kitabuni -- hao anawalaani Mwenyezi Mungu, na wanawalaani kila wenye kulaani. ."
Kukataa ukweli kutaleta matatizo kwa jamii. Wale wanaosema ukweli huishi maisha ya uaminifu, lakini wale wanaokataa au kuficha ukweli wanazua shaka kwa wengine. Wengine wanaweza kutumia vibaya nukta hii hata ikiwa inahusiana na suala lisilo muhimu.
Kuikataa haki ni dhambi kubwa na adhabu yake kwa wale wafanyao hivyo ni kulaaniwa na Mwenyezi Mungu na watu isipokuwa watubu na kurekebisha tabia zao. " Ila wale walio tubu na wakatengeneza na wakabainisha, basi hao nitapokea toba yao, na Mimi ni Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu. Hakika walio kufuru na wakafa hali ni makafiri, hao iko juu yao laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote." (Surah Baqarah, aya ya 160-161)
Ni wazi kuwa kunwa wanadamu wengi ambao hawapati nafasi ya kutubu.