IQNA

Jibu kwa Jinai za Israel

Wapalestina wapongeza operesheni ya Quds iliyotoa pigo kwa muundo wa usalama wa Israel

15:59 - November 24, 2022
Habari ID: 3476138
TEHRAN (IQNA0- Makundi mbalimbali ya Palestina yamesema kuwa, operesheni za kishujaa iliyofanywa dhidi ya utawala wa Kizayuni katika mji wa Baytul Muqaddas ni fakhari kwa taifa la Palestina, ni katika kujibu jinai za Wazayuni na ni kufeli muundo wa kiusalama wa Israel kukabiliana na wanamapambano wa Palestina.

Jumatano asubuhi, kumetokea miripuko miwili katika kituo kikuu cha mabasi na kwenye barabara kuu ya Ramot, magharibi mwa mji wa Baytul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Mzayuni mmoja ameangamizwa na 22 wamejeruhiwa huku hali ya watano kati yao ikiwa mahututi.

Harakati ya Jihad al Islami ya Palestina imesema katika taarifa yake kwamba, opereseheni hiyo ya Quds inayokaliwa kwa mabavu na Israel, ni majibu ya haki ya Wapalestina kwa jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina.

Kamati za Muqawama wa Wananchi wa Palestina nazo zimelipongeza taifa la Palestina kwa operesheni hizo na kusema kuwa, zimefanyika ili kuonesha taifa lote la Palestina limeshikamana vilivyo na mashahidi wao pamoja na mateso wanayopata mateka wa Kipalestina katika makucha katili ya utawala wa Kizayuni wa Israel. 

Kwa upande wake, Harakati ya Demokrasia kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina imepongeza opereseheni hizo za kishujaa za wanamapambano wa Palestina na kusisitiza kuwa hayo ni majibu ya haki ya taifa linalodhulumiwa kila upande la Palestina.

Kabla ya hapo pia, Abdul Latif al Qanoo, msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Paelstina naye alikuwa amelipongeza taifa la Palestina kwa opereseheni hiyo ya kishujaa na kusisitiza kuwa, ugaidi wa utawala wa Kizayuni utaendelea kupata majibu kama hayo ya kishujaa kutoka kwa wanamapambano wa Kipalestina.

4101722

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha