IQNA

Jinai za Israel

Hamas yawataka Wapalestina kuzidisha mapambano dhidi ya Wazayuni wavamizi

18:12 - November 18, 2022
Habari ID: 3476110
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina Hamas ametoa wito kwa wananchi wa Palestina kuzidisha mapambano yao dhidi ya Wazayuni wavamizi wanaokalia ardhi za Palestina kwa mabavu hasa mji Al-Quds (Jerusalem) ili kuulinda Msikiti wa Al-Aqsa ulio mjini humo.

Mohammed Hamada, msemaji wa Hamas huko Al-Quds, alisema kuwepo kwa Wapalestina katika uwanja wa Msikiti wa Al-Aqsa kutasaidia kuzima njama za utawala wa Israel.

Huku akibainisha kuwa mitakaba iliyotiwa saini na baadhi ya tawala za Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel kumeupa kiburi utawala huo ghasibu na hivyo kuufanya uendeleza kutekeleza jinai zake dhidi ya Al-Aqsa na Al-Quds, ametoa wito kwa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kuuunga mkono mji huo mtakatifu na msikiti huo.

Wakati huo huo, Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa imepasisha azimio ikitambua haki ya watu wa Palestina ya kuamua hatima yao wenyewe.

Rasimu ya azimio hilo iliwasilishwa na Misri ikishirikiana na serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika Umoja wa Mataifa, kwa niaba ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC).

Azimio hilo limeungwa mkono na nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Mataifa, zikiwemo nchi za Umoja wa Ulaya, nchi za Amerika ya Kusini, Asia na Afrika, na linatarajiwa kuwasilishwa kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuidhinishwa katikati ya mwezi ujao wa Desemba.

Nchi 167 zilipiga kura ya kuunga mkono azimio hilo, nchi 5 zimepinga na nchi 7 hazikupiga kura.

Riyad al-Maliki, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amezishukuru nchi zilizopiga kura ya kuunga mkono azimio hilo na kusema: Haki ya kujitawala ndio msingi wa haki zote hususan kwa watu wa Palestina ambao wamekuwa chini ya uvamizi wa kikoloni wa muda mrefu wa utawala wa kibaguzi.

Vilevile amepinga misimamo ya nchi zilizopiga kura ya kulipinga au ambazo hazikupiga kura na kusisitiza kuwa, nchi hizo haziwezi kuendelea kuunga mkono utawala vamizi na jinai zake, na hatua zao zitazidisha kiburi na uhalifu wa utawala huo.

4100466

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha