IQNA

Jinai za Israel

Utawala katili wa Israel waendelea kuwaua Wapalestina kiholela

22:35 - December 01, 2022
Habari ID: 3476181
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Afya ya Palestina imetoa ripoti yake na kusema kuwa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2022 hadi hivi sasa, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshaua shahidi Wapalestina 205 katika sehemu mbalimbali za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Wizara ya Afya ya Palestina aidha imesema kwenye ripoti yake hiyo ya jana Jumanne kwamba, wanajeshi makatili wa Israel wamefanya jinai nyingine kubwa, mbali na kuwaua shahidi Wapalesina hao 205.

Imetoa ufafanauzi katika ripoti yake hiyo kwa kusema, Wapalestina 153 wameuliwa shahidi na Israel katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na 52 wameuliwa shahidi na Wazayuni makatili katika eneo la Ukanda wa Ghaza.

Kiujumla Wazayauni hawasiti kufanya jinai yoyote ile dhidi ya Wapalestina alimradi tu wafanikishe malengo yao haramu ya kuendelea kuzikalia kwa mabaru ardhi za Palestina.

Kwa upande wake, Msemaji wa Harakati ya Jihad al Islami ya Palestina, Tariq Ezzeddine hivi karibuni alilaani jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina na kusema kuwa, wanamapambano wa Palesitna watalipa kisasi cha jinai zote zinazofanywa na Wazayuni, iwe hivi sasa au wakati ujao, lakini lazima Wazayuni walipe damu wanazozimwaga za Wapaelstina.

Kwa zaidi ya miaka 70 sasa Wapalestina wanakandamizwa na wananyimwa haki zao. Katika miaka hiyo, utawala wa Kizayuni umefanya jinai kubwa mno dhidi ya Wapalestina, jinai na ukatili ambao ni nadra sana umewahi kushuhudiwa katika kurasa za historia.

3481483

Kishikizo: palestina ، israel ، jinai za israel
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha