IQNA

Jinai za Israel

Misikiti miwili ya Al-Khalil yaharibiwa na walowezi wa Israel

21:18 - November 20, 2022
Habari ID: 3476121
TEHRAN (IQNA) – Walowezi wa Kizayuni wameshambulia misikiti miwili na kuvunja madirisha wakati wa shambulio katika kitongoji cha Bab al-Zawiya katika mji unaokaliwa wa Al-Khalil (Hebron) unaokaliwa kwa mabavu na Israel katika Ukingo wa Magharibi.

Vyombo vya habari vya Palestina vinasema walowezi waliokuwa na silaha nyingi wanaolindwa na wanajeshi wa Israel leo Jumapili wameishambulia misikiti hiyo miwili walipokuwa wakifanya maandamano ya uchochezi katika kitongoji hicho, huku wakiwalenga Wapalestina kwa kelele za matusi na kauli mbiu za ubaguzi wa rangi.

Mapema leo pia Wapalestina kadhaa walipata majeraha katika shambulio lililofanywa na walowezi wa Israel katika kitongoji cha Tel Rumeida mjini humo. Walowezi hao walirushia mawe na chupa tupu majumbani na kuwashambulia na kuwapiga wakazi wa Palestina, na kuwajeruhi baadhi yao.

Vikosi vya uvamizi vya Israel vilivyoandamana na walowezi hao katika mashambulizi yao pia vimewakamata vijana wawili wa Kipalestina wakiwa mbele ya nyumba zao katika kitongoji hicho.

Walowezi pia walishambulia vibanda vya wachuuzi na wapita njia walipokuwa wakipita kwenye vichochoro vya kitongoji hicho, wakiungwa mkono na kulindwa na jeshi katili la Israel.

Mji wa wa kale wa Al Khalil umekuwa sehemu ya ghasia za walowezi wa Kizayuni katika wiki chache zilizopita, huku mashambulizi yakiripotiwa huko karibu kila siku.

3481327

captcha