IQNA

Jinai za Israel

Wapalestina walaani njama za Kuyahudisha mtaala wa shule mjini Quds

21:11 - November 10, 2022
Habari ID: 3476068
TEHRAN (IQNA) – Wapalestina wanaendelea kulaani vikali njama za utawala haramu wa Israel za Kuyahudisha na kupotosha ukweli katika vitabu vya shule katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwamabavu na utawala huo.

Kamati ya Quds ya Baraza la Wananchi la Wapalestina Nje ya Nchi imelaani mitaala potofu ya Israel iliyowekwa kwa wanafunzi wa Kipalestina katika mji wa Quds.

Hoi ilikuja kufuatia usambazaji wa vitabu ambavyo ni pamoja na habari za uwongo kuhusu Palestina na  kupendelea utawala bandia wa  Israeli katika Shule za Al Eman.

Katika taarifa, kamati hiyo ilisema kwamba usambazaji wa vitabu hivi unamaanisha kuwa shule "inashiriki katika mchakato wa Kuyahudisha elimu ya Wapalestina na inakiuka utamaduni wa wanafunzi wa Kipalestina ambao wanafutiliwa mbali ustaarabu wao."

Wazazi wa wanafunzi katika shule hizo wameafikiana na uongozi wa Shule za Al Eman kwamba vitabu vya Israel havitakubaliwa, lakini shule hizo zilikubali mitaala hiyo ya Kiyahudi  kufuatia shinikizo kutoka kwa mamlaka ya uvamizi ya Israel.

Mnamo Julai, utawala haramu wa Israeli ulifuta leseni za shule ambazo zilikataa mitaala yenye kufuata mitaala ya Kiyahudi.

Katika miongo ya karibuni, utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel umechukua hatua nyingi kwa lengo la kuubadilisha utambulisho wa Kiislamu wa Quds tukufu hasa kupitia ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kubadilisha mitaala ya shule.

Desemba 23, 2016 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio 2334 ambalo liliutaka utawala haramu wa Israel usimamishe haraka na kikamilifu shughuli zote za ujenzi wa vitongoji katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu.

Utawala wa Kizayuni ambao unaungwa mkono kikamilifu na Marekani katika hatua zake hizo haramu umekaidi maazimio ya Umoja wa Mataifa na umedhamiria kubadilisha muundo wa kijiografia na kidemografia wa maeneo ya Palestina; ili kwa kuyahudisha maeneo hayo, kuhakikisha unazihodhi na kuzidhibiti kikamilifu ardhi za Wapalestina.

3481199

captcha