IQNA

Ukweli katika Qur'ani Tukufu / 9

Muujiza wa kisayansi katika Qur'ani Tukufu kuhusu mimea

21:02 - December 10, 2022
Habari ID: 3476226
TEHRAN (IQNA) – Hussein Fadhil al-Hulw, mwanazuoni wa Kiarabu, katika makala ameorodhesha maudhui ya baadhi ya aya za Quran kuhusu ukuaji wa mimea yamethibitishwa na sayansi ya kisasa.

Dondoo za makala hiyo ni kama ifuatavyo:

Aya ya 99 ya Surah Al-An’am inazungumzia kukua kwa mimea: “Na Yeye ndiye anaye teremsha maji kutoka mbinguni; na kwayo tunatoa mimea ya kila kitu. Kutokana na baadhi yao tukatoa mimea ya majani, tukatoa ndani yake punje zilizo pandana; na kutokana na mitende yakatoka kwenye makole yake mashada yaliyo inama; na bustani za mizabibu na mizaituni, na makomamanga, yaliyo fanana na yasiyo fanana. Angalieni matunda yake yanapo zaa na yakawiva. Hakika katika hayo pana Ishara kwa watu wanao amini."

Ukweli kwamba maji ni dutu ya msingi kwa ukuaji wa mimea yote ni ya kushangaza. Wakati wa mvua, maji huchanganyika na mchanga na mvuto na nguvu za kukataa zinaundwa kati ya chembe ndogo za maji na mchanga. Matokeo yake, mchanga huongezeka kwa kiasi. Huu ni ukweli wa kisayansi ambao tunaujua leo lakini hakuna aliyeujua  wakati Qur'ani Tukufu ilipoteremshwa.

Katika aya nyingine, Qurani inasema: “…Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakini tunapo yateremsha maji juu yake husisimka na kututumka, na kumea kila namna ya mimea mizuri. (Surah Al-Hajj, Aya ya 5)

Katika ardhi kavu harakati hazisiti kamwe. Hata chembe kwenye mchanga husogea ingawa harakati hizo huwa ni dhaifu. Maji yanapofikia mchanga mkavu, huhifadhiwa humo kwa muda mrefu ili kukidhi kiu ya mimea.

Aya hii inazungumza juu ya hatua za kuota kwa mmea. Inaanza na mvua, kisha maji huchanganyika na chembe za mchanga na huandaa mazingira ya kuchipua mbegu. Wakati mbegu iliyo katika mchango inapopata majai  huanza kuota. Qur'ani Tukufu imezielezea hatua hizi ifutavyo: "tunapo yateremsha maji juu yake husisimka na kututumka."

captcha