IQNA

Ukweli Katika Qur’ani Tukufu /3

Ukweli kuhusu uhusiano kati ya imani dhaifu na kujiua

20:22 - November 14, 2022
Habari ID: 3476088
TEHRAN (IQNA) – Tafiti za kisayansi zinathibitisha kwamba wasiomuamini Mwenyezi Mungu ndio watu walio hatarini zaidi na ndio wanaokata tamaa maishani na hivyo kiwango cha kujiua miongoni mwao ni kikubwa sana.

Katika makala iliyopewa jina la “Kumkana Mwenyezi Mungu, Kujiua na Nguvu ya Mafundisho ya Kiislamu”, mtafiti Abduldaem Al-Kaheel anaashiria utafiti wa kisayansi ambao unathibitisha kiwango kikubwa cha kujiua miongoni mwa watu wasioamini kuwa kuna Mungu ikilinganishwa na wafuasi wa dini.

Wasiomuamini Mwenyezi Mungu kwa muda mrefu wamesisitiza mawazo na uhuru wao na wamewasilisha vipengele hivi kama tofauti zao na waumini, na hivyo, wanajiona kuwa wenye furaha zaidi kuliko wengine.

Lakini uchunguzi wa hivi majuzi unaonyesha kwamba watu wasiomuamini Mwenyezi Mungu ndio walio na kiwango kikubwa zaidi cha mfadhaiko wa moyo. Katika utafiti huu, imethibitishwa kwamba kiwango cha juu zaidi cha kujiua kilikuwa miongoni mwa watu wasioamini kuwepo Mwenyezi  Mungu hayuko au wale ambao si  wafuasi wa wa dini yoyote na wanaishi bila lengo na bila imani.

Uchunguzi wa kisayansi unaohusiana na kujiua umethibitisha kwamba kiwango cha juu zaidi cha kujiua kiko katika nchi ambazo wakazi wake wengi hawamuamini Mwenyezi Mungu, na hapa Uswidi inaongoza kwani  ina kiwango cha watu wasiomuamini Mwenyezi Mungu.

Uchunguzi wa kisayansi unathibitisha kwamba mafundisho ya kidini yana jukumu kubwa katika kupunguza majaribio ya kujiua. Katika suala hili, Uislamu umeweka mafundisho yenye nguvu zaidi na umetoa maonyo dhidi ya kujiua.

Kwa mujibu wa vyanzo vya mafundisho ya Kiislamu kama vile Sahih ya Bukhari na Sahih ya Muslim, Mtume Muhammad (SAW) amewaonya waziwazi waumini dhidi ya kujiua, akisema, "Yeyote anayejiua kwa chochote katika dunia hii atateswa nacho Siku ya Hukumu. ” Mtukufu Mtume (SAW) anabainisha zaidi kwamba yeyote anayejitupa chini kutoka kwenye mlima na kujiua basi atakuwa amejitupa kwenye Moto wa Jahannamu milele na milele, yeyote anayekunywa sumu na kujiua atakuwa anaivuta kwenye Moto wa Jahannam milele na milele na yeyote anayejiua kwa kipande cha chuma atakuwa na chuma hicho mkononi mwake, na kukiingiza tumboni mwake katika Moto wa Jahannam milele na milele.

Hadith pia inaashiria kunywa sumu na kuitupa kutoka mahali pa juu kama njia nyingine ya kujiua. Kwa hiyo, Uislamu haujapuuza jambo hili hatari na umelishughulikia.

Kulingana na tafiti, kiwango cha kujiua kimeongezeka sana katika miaka hamsini iliyopita, na sio siri kwamba ongezeko hili linaweza kuwa kutokana na kuongezeka kwa kiwango itikadi ya kutomuamini Mwenyezi Mungu katika kipindi hicho.

Nchi ambazo hazitoi sheria dhidi ya kujiua kwa kisingizio cha uhuru wa kusema, kama vile Uswidi na Denmark, ndizo zinazo viwango vya juu zaidi vya kujiua.

captcha