IQNA

Tafsiri za Qur'ani Tukufu na Wafasiri /12

Ruh Al-Ma’ani; Tafsiri kubwa zaidi ya Qur'ani ya manachuoni wa Kisunni

22:16 - December 20, 2022
Habari ID: 3476278
TEHRAN (IQNA) – Ruh al-Ma'ani ni tafsiri pana na kamili zaidi wa Qur'ani Tukufu hadi sasa iliyoandikwa na wanazuoni wa Kisunni.

Ina  maoni ya tafsiri zilizotangulia na inaweza kuchukuliwa kuwa mukhtasari wa tafsiri za Qur'ani zilizoandikwa hapo awali.

Ruh al-Ma'ani fī Tafsiri-l-Qur'ani-l-'Aẓīm wa Sab'u-l-Mathani , iliyoandikwa na Mahmoud bin Abdullah al-Alusi ni tafsiri ya Qur'ani Tukufu katika lugha ya Kiarabu. Ni tafsiri ya Qur'ani yenye msingi wa kiakili na Ijtihad kwa kutumia mbinu ya kifasihi.

Ni tafsiri pana na kamili zaidi ya Qur'ani iliyoandikwa kwa njia ya zamani baada ya ile ya Fakhr Razi na inaweza kuchukuliwa kuwa juzuu ya pili ya tafsiri hiyo. Imechapishwa katika juzuu 16 na kwa hakika Ruh al-Ma’ani ni tafsiri yenye muundo ensaiklopidia.

Kuhusu Mwandishi

Abu al-Thana’ Shihab ad-Din Sayyid Maḥmud ibn ‘Abd Allah al-Ḥusaynī al-Alusi al-Baghdadi (1802-1854) alikuwa Faqihi (mwanasheria), mkalimani, bingwa wa fasihi na mwanachuoni wa kidini huko Baghdad. Alisoma fasihi na baba yake na wataalamu kadhaa tangu utotoni na akafanya maendeleo makubwa kutokana na ufahamu wake wa juu na kumbukumbu nzuri.

Muda si mrefu akawa mwanachuoni wa juu na alipata lakabu ya Allamah. Alikuwa mfuasi wa madhehebu ya Shafi’i lakini mwaka 1832 na baada ya kujifunza kuhusu Fiqh ya madhehebu mengine akawa mfuasi wa fiqhi ya Hanafi.

Anaandika katika utangulizi wa tafsiri yake kuwa tangu utotoni alikuwa ana hamu sana ya kugundua siri za Qur'ani Tukufu na alimuomba Mwenyezi Mungu amsaidie katika njia hii.

Alitumia miaka yake ya awali na ujana wake kusoma kuhusu Qur'ani Tukufu na aliandika kitabu kiitwacho Daqaiq at-Tafsir kuhusu maswali yanayohusiana na Qur'ani Tukufu.

Akiwa na umri wa miaka 43 alianza kuandika tafsiri yake ya Qur'ani Tukufu na akaimaliza mwaka 1850, ambapo aliipa anuani ya Ruh al-Ma'ani fī Tafsiri-l-Qur'ani-l-'Aẓīm wa Sab'u-l-Mathani.

Nukta kadhaa kuhusu tafsiri ya Qur'ani ya Ruh Al-Ma’ani

Ruh al-Ma’ani ndio tafsiri pana na kamili zaidi ya Qur'ani Tukufu ambayo hadi sasa imeandikwa na mwanazuoni wa Ahul Sunna wal Jamaa. Kimsingi tafsiri hii inajumuisha  maoni ya tafsiri zilizotangulia na inaweza kuchukuliwa kuwa mukhtasari wa tafsiri za Qur'ani zilizoandikwa hapo awali. Al-Alusi ametumia maoni yaliyotajwa katika tafsiri za Qur'ani kama kama vile za Ibn Atiyya, Abu Hayyan. Kashshaf, Abu al-Saud, Baizawi, na Fakhr Razi. Ametaja maoni yao na pia amazihakiki tafsiri walizoandika. Amenufaika zaidi na kazi ya Fakhr Razi.

captcha