IQNA

Tafsiri na Wafasiri wa Qur'ani Tukufu /14

Tafsiri yenye muelekeo wa utafiti kuhusu Muujiza wa Balagha wa Qur'ani Tukufu

21:14 - January 11, 2023
Habari ID: 3476386
TEHRAN (IQNA) – Sayed Radhi katika kitabu chake ‘Talkhis al-Bayan fi Majazat al-Quran’ anazungumzia muujiza wa Qur'ani Tukufu kwa mtazamo balagha na sitiari.

‘Talkhis al-Bayan fi Majazat al-Quran’ ni tafsiri ya Qur’ani ya madhehebu ya Shia ambayo ina mtazamo mpya wa tafsiri ya Qur’ani. Katika kazi hii, Sayed Radhi alitumia ujuzi wake na maarifa yake mengi kuandika kitabu cha kwanza juu ya mafumbo na sitiari katika Qur'ani Tukufu. Kitabu hiki chenye juzuu moja kinahusu ufasiri wa aya, maneno, istilahi na tamathali za semi katika Qur'ani Tukufu

Kitabu hiki  kimezingatiwa kuwa moja ya kazi kuu za kitaalamu zilizoandikwa katika karne ya 4 Hijri kwani kinataja tamathali za semi na kutoa mifano kutoka katika mashairi ya Kiarabu.

Kitabu kinaangazia vipengele tofauti vya muujiza wa balagha na ufasaha wa Qur'ani Tukufu. Ufasaha unamaanisha kuwa fasaha na ushawishi katika kuzungumza au kuandika na kuzingatia hadhi ya anayelengwa

Sayyed Radhi alikuwa nani?

Mohammad Ibn Hussein ibn Musa, anayejulikana kama Sayed Radhi (969-1015) alikuwa mwanazuoni wa Kishia na alikuwa kaka yake Sayed Mortadha. Alishikilia nyadhifa kadhaa kuu, zikiwemo hakimu na mkuu wa msafara wa Hija wakati wa utawala wa ukoo wa Buyid. Aliandika vitabu vya Kiislamu na tafsiri ya Qur'ani Tukufu pamoja na kitabu cha mashairi. Kazi yake kuu ilikuwa ni kukusanya Nahj al-Balagha. Pia alianzisha shule ambayo wengine wanasema ndiyo shule ya kwanza ya kufundisha sayansi za kidini.

Alisoma kwa Muhammad Tabari Maliki, Abu Abdullah Jurjani, Faqih Hanafi, Qadhi Abdul Jabbar, na Akfani Qadhi.

Katika Talkhis al-Bayan fi Majazat al-Quran, Sayed Radhi anataja maoni tofauti kulingana na Qiraa saba, kisha akajadili maana za maneno na kutoa maoni yake kuhusu masuala ya maadili. Pia ananukuu Hadith katika kuzungumzia vipengele vya balagha vya Qur'ani Tukufu.

Mada ya kwanza iliyotajwa katika kitabu hicho ni kuhusu aya ya 7 ya Sura Al-Baqarah: “Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa.” Anasema ‘muhuri’ ni sitiari kwa sababu mnafiki hutembeza macho yake na kuona mambo lakini hajifunzi kutokana nayo.

Mada ya mwisho ni kuhusu aya ya 1 hadi 3 ya Surah Al-Inshirah “Je,  Hatukukunjulia kifua chako? Na tukakuondolea mzigo wako. Ulio vunja mgongo wako?

Sayid Radhi anasema maneno yaliyolemea mgongo wako ni sitiari ya matatizo na magumu aliyopitia Mtume Muhammad SAW (SAW) wakati wa utume wake.

Kitabu hiki kimechukuliwa kuwa chanzo muhimu na wafasiri wa Qur'anI Tukjufu baada ya Sayed Radhi na wametumia maudhui yake katika kazi zao.

captcha