IQNA

Harakati za Qur'ani Sudan

Waliohifadhi Qur’ani Tukufu nchini Sudan wapongezwa na wananchi + video

19:37 - January 13, 2023
Habari ID: 3476399
TEHRAN (IQNA)- Idadi kubwa ya wananchi wameshiriki katika sherehe ya kuwapongeza wanafunzi wanafunzi 150 waliohifadhi Qur'ani katika shule za mji wa Hamshkorib Kaskazini-Mashariki mwa Sudan.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, klipu za mahudhurio makubwa ya wananchi katika sherehe za kuhitimu wanafunzi 150 wa Qur'ani Tukufu wa shule za mji wa Hamshkorib zimeenea katika mitandao ya kijamii.

Maafisa wa shule za kuhifadhi Qur'ani katika mji wa Hamshkorib waliandaa matembezi ya Qur'ani huku kukiwa na mahudhurio makubwa ya watu walioshiriki katika sherehe za mahafali ya waliohifadhi  Qur'ani.  Wengi wamezitaja shule za Qur'ani nchini Sudan zinazoitwa "Khalawi" nchini humo kuwa ni kituo muhimu zaidi cha kudumisha nafasi ya Qur'ani Tukufu nchini Sudan.

Watumiaji wa mitandao pia wamechapisha picha za mtoto wa umri wa miaka 9 akihifadhi Qur'ani Tukufu katika sherehe hii, ambaye anasoma Qur'ani Tukufu kwa usahihi kwa kufuata sheria za Tajweed.

Shirika la Habari la Sudan (Suna) limeripoti kuwa hafla hii ilifanyika mbele ya gavana wa Al-Qadarif, mkuu wa shule za kuhifadhi Qur'ani na maafisa wengine kadhaa wa serikali.

Sheikh Al-Amin Hamid, mwakilishi wa shule za Hamshkourib huko Al-Qadarif, alielezea fahari yake katika kuhitimu kwa wahifadhi 150 wa Qur'ani Tukufu. Kwa upande mwengine mkuu wa mkoa huu alitangaza kuanzisha kituo cha mafunzo ya ufundi stadi chenye mafungamano na shule hizo kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi wa Qur’ani Tukufu na kuwataka waendelee na elimu ya umma.

4114228

captcha