Katika mkusanyiko huo mkubwa wa Qur'ani, washiriki waliojumuika kwa kauli mbiu kuu "Tunaiunga mkono Palestina" na huku wakitoa nara ya "Allahu Akbar," walieleza uungaji mkono wao kwa Wapalestina wanaodhulumiwa wa Gaza na kulaani mauaji ya kimbari yanayoendelezwa na utawala haramu wa Israel.
Miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo alikuwemo Sheikh Talal Abdulrahman, mfungwa wa zamani wa Kipalestina aliyeshikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni wa Isarel kwa muda mrefu, ambaye aliwasilisha salamu za wapiganaji wa Kipalestina kutoka katikati ya medani ya vita kwa vijana shupavu wa Iran.
"Washiriki wa mkusanyiko huu mkubwa wa Qur'ani sasa wamekusanyika ili kutangaza upya utii wao kwa Mtume Muhammad (SAW)," alisema na kuongeza, "Kwa mkusanyiko huu mkubwa, mumeonyesha kuwa nyini ni waaminifu kwa dini ya Kiislamu, neno la Mwenyezi Mungu, na neno la Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW).
Maqari mashuhuri na watangazaji wa kipindi cha televisheni cha Mahfel ambao ni Ahmad Abolqasemi, Sayyid Hassanayn al-Hulw, Hamed Shakernejad, Hujjatul Islam Gholamrridha Qasemian, na Ridhwan Darwish, walisoma Qur'ani katika hafla hiyo.
Mahfel, kipindi cha Televisheni cha Qur'ani ambach hurushwa na Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, huwavutia mamilioni ya watazamaji ambao hujumuika kukitazama kabla tu ya kufuturu ili kusikiliza Qur'ani Tukufu.
Siku ya 17 ya Rabi al-Awwal, ambayo inaadhimishwa Septemba 21 mwaka huu, inaaminika na Waislamu wa madhehebu ya Shia kuwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Mohammad (SAW), huku Waislamu wa madhehebu ya Sunni wakizingatia siku ya 12 ya mwezi (Septemba 16 mwaka huu) kama siku ya kuzaliwa Mtume wa Mwisho (SAW)
Hayati Mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Khomeini (RA) alitangaza kipindi baina ya tarehe hizo mbili kuwa kuwa Wiki ya Umoja wa Kiislamu ili badala ya kuwepo mvutano kuhusu tarehe, Waislamu wazingatie masuala muhimu zaidi ya umoja baina yao.
359956