IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Majeshi ya Iran na Oman kufanyika Tehran

19:43 - May 12, 2016
Habari ID: 3470308
Mashindano ya 7 ya kirafiki ya Qur'ani baina ya majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Ufalme wa Oman yatafanyika hivi karibuni mjini Tehran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Hujjatul Islam Ali Reza Zamyar, afisa katika kamati andalizi ya mashindano hayo amesema yatafanyika Mei 15-16.

Ameongeza kuwa mashindano hayo ya siku mbili yatafanyika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini Iran.

Halikadhalika amebaini kuwa Majeshi ya Iran yatakuwa na washiriki 14 waliohifadhi Qur'ani na wataksoma tajweed na kwamba Jeshi la Oman nalo pia litakuwa na idadi sawa na hiyo.

Mashindano hayo yatakuwa na kategoria za kuhifadhi Qur'ani Kikamilifu Juzuu 20, 10 na tano.

Mashindano hufanyika kila mwaka ima nchini Iran au Oman kwa lengo la kuimarisha urafiki baina ya majeshi ya nchi hizi mbili jirani na za Kiislamu.

3497172

captcha