IQNA

Mawaidha

Qur’ani Tukufu Inasemaje kuhusu Usiku wa Qadr?

20:24 - April 11, 2023
Habari ID: 3476850
TEHRAN (IQNA) – Baadhi ya aya za Qur’ani Tukufu zinahusu Usiku wa Qadr (Laylatul Qadr) na zinaweza kutusaidia kutambua hadhi muhimu ya usiku huu iwapo tutazingatia.

Haya ni kwa mujibu wa mwanazuoni wa Chuo Kikuu cha Tehran Majid Maaref, akizungumza katika kongamano la hivi karibuni katika Chuo Kikuu cha Madhehebu za Kiislamu kuhusu hadhi ya Usiku wa Qadr. Hizi ni sehemu za maneno yake kwenye kongamano hilo:

Kuna aya katika Quran zinazozungumzia Usiku wa Qadr. Katika Surah Al-Baqarah, Mwenyezi Mungu anasema: " Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge..." (Aya ya 185)

Ili kubainisha kama Qur'an Tukufu iliteremka usiku mmoja au usiku tofauti, Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 3 ya Surah Ad-Dukhan, "Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji."

Ili kuonesha umuhimu wa usiku huu uliobarikiwa, Sura nzima, yaani Sura Al-Qadr, imeteremshwa kuhusu hilo: “Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu. Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri? Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu. Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo. Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.” (Aya ya 1-5)

Aya ya 3 inaonyesha thamani ya usiku huu, ambao ni bora kuliko miezi elfu. Kisha Mwenyezi Mungu anasema malaika wanashuka usiku huu.

Kuna Aya nyingine inayozungumzia usiku huu wa cheo  nayo ni Aya ya 2 ya Surah An-Nahl, ambayo inaonekana kuihusu pia. “Huwateremsha Malaika na Roho kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake ili nyinyi muonye kwamba hapana mungu ila Mimi, basi nicheni Mimi.’” Aya hii inafanana sana na ile iliyo katika Surah Al-Qadr.

Aya ya 2 ya Surah An-Nahl inasema kwamba Mwenyezi Mungu huteremsha Malaika pamoja na Roho ili kubeba amri zake kwa yeyote katika waja Wake Anayemtaka. Aya hii ina nukta ya ziada, na huo ni ukweli kwamba malaika wanashuka juu ya wanadamu sio juu ya kile kisicho na uhai.

captcha