IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Aya za Kila Siku: Qur'ani Tukufu imeteremshwa katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu

11:26 - April 11, 2023
Habari ID: 3476848
Kwa mujibu wa Surat Al-Qadr katika Qur'ani Tukufu, Ramadhani ni mwezi uliobarikiwa ambapo Mtume Muhammad SAW aliteremshiwa Qur'ani Tukufu.

Daily Verses: Quran Revealed on Qadr Night  

Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu.

Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri?

Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu.

Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo.

Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.

captcha