IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu / 73

Pendekezo la Swala ya Usiku katika Surah Al-Muzzammil

14:10 - April 26, 2023
Habari ID: 3476915
TEHRAN (IQNA) - Usiku huwa ni maalumu kwa ajili ya kupumzika lakini amani iliyopo katika siku hizi hupelekea baadhi ya watu kutenga sehemu hiyo kwa ajili ya ibada na kutafakari. Inaelekea kwamba kuabudu wakati wa usiku wa manane huwa na fadhila zake maalumu.

Sura ya 73 ya Qur'ani Tukufu ni Surah Al-Muzzammil. Ina aya 20, Sura hiyo iko katika Juzuu ya 29 ya Qur'ani Tukufu. Ni Sura ya Makki na ya tatu iliyoteremshwa kwa Mtume Muhammad (SAW).

Jina la Sura limetokana na neno katika Aya yake ya kwanza linalomtaja mtu ambaye amejifunika kwa nguo. Inaelekea kwamba aya inamuashiria Mtume Muahmmadswali kwamba aya zinamzungumzia Mtume Muhammad (SAW) alikuwa amesumbuliwa na makafiri. Aya ya pili inasema, “ Kesha usiku kucha, ila kidogo tu!.”

Sura hii inamualika Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) kuabudu usiku, kusoma Qur'ani, na kuwa na subira mbele ya makafiri kwani pia inazungumzia Siku ya Kiyama.

Kwa mujibu wa Sura, jukumu zito linamngoja Mtukufu Mtume (SAW) kama ilivyotajwa katika aya ya 5: “Hakika Sisi tutakuteremshia uli nzito.” Baadhi ya wafasiri wanasema kwamba “neno” linaashiria kuteremshwa Qur'ani Tukufu.

Pendekezo hili ingawa, si maalum kwa Mtume Muhammad (SAW) pekee bali ni la waumini wote kwani linajaribu kuwahimiza kumwabudu Mungu usiku. " Hakika kuamka usiku kunawafikiana zaidi na moyo, na maneno yake yanatua zaidi." (Kifungu cha 6)

Sura hiyo pia inamtaka Mtukufu Mtume kuwa na subira mbele ya dhiki kutoka kwa maadui na ajiepushe na wale wanaomwita mwendawazimu au mshairi. Tena, hii si amri makhsusi kwa Mtume bali ni kwa waumini wote. Baada ya kuwaonya makafiri, Sura pia inawahimiza waumini kufanya subira.

Moja ya aya za Sura inahusu namna sahihi ya usomaji wa Quran. Aya ya 4 ya Sura inawahimiza Waislamu kusoma Qur'ani Tukufu kwa sauti za polepole, zilizopimwa.

captcha