Ulimwengu huo umeumbwa kwa kutegemea mwenendo na matendo ya watu, na kwa kuzingatia matendo hayo, watagawanyika katika makundi mawili ya watu wema na waovu na kila moja litakuwa katika nafasi tofauti.
Haya ni miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa katika Surah Al-Muddaththir. Ni sura ya 74 ya Qur'ani Tukufu ambayo ina aya 56 na iko katika juzuu ya 29.
Ni Makki na ni Sura ya 4 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW). Imeteremshwa katika miezi ya mwanzo baada ya Muhammad (SAW) kuteuliwa kuwa utume.
Neno Muddaththir maana yake ni 'aliyevaa nguo' na linamrejelea Mtukufu Mtume (SAW).
Katika aya za mwanzo za Sura, Mwenyezi Mungu anamtaka Mtukufu Mtume (SAW) asimame na kutoa onyo lake kwa watu.
Sehemu nyingine ya Sura ni kuhusu mtu aliyemwita Mtume (SAW) kuwa ni mchawi. Mwenyezi Mungu anaangazia ukuu na hadhi ya juu ya Qur'an na anawatishia wale wanaouita uchawi: " Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar." (Aya ya 26)
Kwa mujibu wa Allamah Tabatbaei, katika Tafsiri yake ya Qur'ani ya Al-Mizan, sura hii ina dhamira kuu tatu. Kwanza inamuamuru Mtukufu Mtume (SAW) kunyanyuka na kuwaonya watu. Amri hiyo imetolewa kwa namna inayoonyesha kuwa ni miongoni mwa amri za kwanza baada ya kuteuliwa utume. Pili, inaangazia ukuu na hadhi ya juu ya Qur'ani Tukufu. Na ya tatu, Sura inawatishia wale wanaoikadhibisha Qur'ani Tukufu na kuiita uchawi, na inawakemea wanaokataa wito wa Mwenyezi Mungu.
Sura pia inazungumzia sifa za watu wa Peponi na watu wa Motoni.
Inataja mazungumzo kati ya vikundi viwili. Watu wa peponi wanawauliza kundi jingine kwa nini waliishia kwenye moto na wanataja sababu nne.
“‘Ni nini kilicho kupelekeni Motoni?’ Waseme: Hatukuwa miongoni walio kuwa wakisali. Wala hatukuwa tukiwalisha masikini. Na tulikuwa tukizama pamoja na walio zama katika maovu. Na tulikuwa tukiikanusha siku ya malipo. Mpaka yakini ilipo tufikia.” (Aya za 42-47)